Madawa ya kulevya
Question
Ipi hukumu ya kutumia madawa ya kulevya
Answer
Kisharia ni haramu kutumia madawa ya kulevya ya aina zake zote na kwa majina yake tafauti, kwani Sharia yote inakusudia na kulenga kulinda akili na kuikinga na vile vinavyoiondoa, ukiongezea na kunapelekea kwake madhara makubwa kiafya kiakili na kijamii, ama kufanya biashara ya madawa hayo kunapelekea kiwango cha kuwa katika makosa makubwa, kwani kunasababisha uharibifu kwa mwanadamu na kumvurugia maisha yake, lakini pia kunapelekea madhara makubawa kwa jamii na nchi.
Mwenyezi Mungu Mtukufu Anajua zaidi.