Sadaka yenye kuendela
Question
Ni zipi aina ya Sadaka zenye kuendelea?
Answer
Aina ya Sadaka zenye kuendelea ambazo kunasihi kuweka mali kwa njia ya sadaka yenye kuendelea ni nyingi na nyepesi, Sadaka yenye kuendelea ni katika matendo mema, na ibada za kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na zinamfaa maiti baada ya kuondoka katika katika maisha ya Dunia’Mtume S.A.W. anasema: Anapofairki mwanadamu matendo yake hukatika, isipokuwa vitu vitatu; Sadaka yenye kuendelea, au elimu inayopatiwa manufaa, au mtoto mwema anayemuombea dua” (Hadithi hii imepokelewa na Muslim). Na Sadaka yenye kuendelea ni Waqfu, na masharti katika waqfu kuwa kitu ambacho kinasihi kuuzwa, na kunufaika nacho kikiwa kinaendelea kubaki, na kutofungamana na haki ya mtu yeyote, na kunajuzu pia kutoa Waqfu kwa mali au chakula kama waonavyo baadhi ya Wanazuoni.