Maana ya sadaka yenye kuendelea
Question
Ni ipi Sadaka yenye kuendelea?
Answer
Sadaka yenye kuendelea ni sadaka inayoendelea vizazi na vizazi, si kizazi kimoja tu, na inajumisha watu wengi, kama kuchapisha msahafu, vitabu vya elimu yenye manufaa, kujenga msikiti, shule, hospitali na eneo la makaburi kwa masikini, kusaiadia miradi ya taifa kama kuvuta maji na umeme na kuwahudumia masikini na mfano wa hayo katika yale ambayo yanafikia malengo ya kudumu na manufaa kwa uma.