Dhana ya bidaa ya upotofu

Egypt's Dar Al-Ifta

Dhana ya bidaa ya upotofu

Question

Ni nini dhana sahihi ya bidaa? Je, kila jambo lisilofanywa na Mtume ni bidaa? 

Answer

Katika lugha neno bidaa hurejelea kitu kipya katika dini baada ya kukamilika, na katika Sharia wataalamu walitoa ufafanuzi wa bidaa kwa dhana mbili; dhana ya kwanza: ya Al-Izz ibnu Abdul-Salaam aliyesema kuwa kila jambo ambalo Mtume (S.A.W.) hakulifanya ni bidaa, akaigawa katika aina: Bidaa iliyo wajibu, bidaa iliyo haramu, bidaa iliyo nzuri, bidaa inayo chukiza na bidaa iliyo halali, na namna ya kutambua na kuainisha bidaa yenyewe ni kuipima kwa kanuni za Sharia basi ikiwa katika kanuni za wajibu huwa wajibu na ikiwa karibu na kanuni za haramu basi huwa haramu na kadhalika.

Dhana ya pili, ni kuhusisha bidaa kwa jambo lisilokubaliwa katika Sharia yaani iliyo haramu tu, na hayo ndiyo maoni ya wanafiqhi wa umma (Al-Jumhuri), na inayotuhusu hapa ni kuelezea dhana ya bidaa iliyokatazwa ambayo huwajibisha dhambi kwa anayeifanya, lakini tuulize; je kila jambo ambalo Mtume (S.A.W.) hakulifanya ni bidaa haramu?

Bila shaka, Hapana ambapo umma walifanya mambo mapya mengi ya heri na mazuri baada ya Mtume (S.A.W.) nayo mambo yote mubaha, kwa hiyo Al-Ghazaly anasema: "Si kila jambo jipya ni haramu, bali linalokatazwa ni bidaa inayopingana na sunna thabiti au hukiuka agizo la kisharia", kwa maana hii, dhana sahihi ya bidaa huwa wazi.

Share this:

Related Fatwas