Uhalali wa sifa na kutohoa.
Question
Ipi hukumu ya kumsifu Mtume S.A.W kutohoa na kuleta kaswida za kidini?
Answer
Katika mambo matukufu na mazuri mja kuelezea upendo wake kwa Mola wake Mtukufu na kwa Mtume wake Mtukufu: Ni kusifu wasifu mzuri, kwani ni dalili ya upendo, na mapenzi ya kweli, kwani mwanadamu kila anapopenda kitu huzidisha zaidi wasifu wake na kumtaja kwake, haukuwa ulimi wa msemaji isipokuwa huelezea ulimi wa hali, na kila kitu huongezeka utukufu kwa wasifu, isipokuwa wasifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kuwasifu hao kwa mwenye kusifu kuna utukufu, bali hakuna yeyote aliyebora kusifiwa zaidi ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake Mtukufu, katika Hadithi ya Al-Aswad Ibn Sarii R.A amesema: Nilisema: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, nimemsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa sifa, na nimekusifa Wewe kwa sifa, Mtume S.A.W akasema:
“Sifia na anza na sifa za Mwenyezi Mungu Mtukufu”. Imepokewa na Imamu Ahmad.