Kuswali Swala ya toba

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuswali Swala ya toba

Question

Nini hukumu ya kuswali Swala ya toba? Na inaswaliwa wakati gani?

Answer

Imepokelewa kutoka kwa Abu Bakr, (R.A), amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akisema: “Hakuna mtu afanyaye dhambi kisha akajitakasa (akatia udhu), kisha akaswali, kisha akamuomba Mwenyezi Mungu msamaha, ila  Mwenyezi Mungu atamsamehe.” Kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) akasoma Aya hii: { Na ambao pindi wafanyapo uchafu au wakajidhulumu nafsi zao humkumbuka Mwenyezi Mungu na wakamwomba msamaha kwa dhambi zao} [Al-Imran: 135] Imepokelewa kutoka kwa Al-Tirmidhiy katika “Sunan” yake.

Hadithi hii inaashiria uhalali wa Swala ya toba, nayo inapendekezwa kwa mujibu wa maafikiano ya madhehebu manne ya kifiqhi. Inapendekezwa kwa Muislamu akifanya dhambi, kutawadha vizuri, kisha aswali rakaa mbili. rakaa ambazo ajitahidi kuuhudhurisha moyo wake na kunyenyekea kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kisha anaomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu humsamehe kwa rehema yake, inapaswa kutimiza masharti ya toba kwa kujutia dhambi na kuazimia kutorejea tena, na kama inahusiana na haki ya binadamu ni kuirudisha kwake haki hiyo. Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye anayejua Zaidi.

Share this:

Related Fatwas