Kusali sala kadhaa wakati mmoja
Question
Ni nini hukumu ya kusali sala kadhaa wakati mmoja?
Answer
Kimsingi, ni wajibu kusali kila sala katika wakati wake maalumu bila ya kusogeza mbele wala kuchelewesha, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {hakika Sala kwa Waumini ni faradhi iliyowekewa nyakati maalumu} [An-Nisaa: 103], kuziunganisha sala pamoja katika wakati mmoja huruhusiwa katika hali maalumu na kwa sababu au udhuru, ambapo miongoni mwa udhuru hizo; mvua mzito inayosababisha mashaka kwa waumini kwenda msikitini, kwani ni ngumu kwenda msikitini kusali wakati wa Alasiri na kwenda tena wakati wa Isha.
Rai inayopendekezwa hapa kwa fatwa katika hali hii ni kwamba inajuzu kuziunganisha sala za Adhuhuri na Alasiri, Maghrib na Isha katika wakati wa inayokuja kwanza kati yao, pasipo na kufupisha rakaa za sala, kwa dalili ya hadithi iliyo katika Bukhary na Muslim kutoka kwa Ibnu Abbas (R.A.) alisema: “Mtume (S.A.W.) alisali katika Madinah Adhuhuri na Alasiri pamoja, Maghrib na Isha pamoja” Muslim aliongeza: “pasipo na hofu wala safari”, Imamu wawili Malik na Al-Shafii (Mwenyezi Mungu Awarehemu) walisema: “Mtume alifanya hivyo kwa sababu ya mvua”