Kuswali Swala iliyopita katika wak...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuswali Swala iliyopita katika wakati uliokatazwa

Question

Je, inajuzu kwa Muislamu kuswali Swala zilizopita katika nyakati ambazo Sharia inakataza kuziswali?

Answer

Haikukatazwa na Sharia kuswali Swala zilizopita katika wakati wowote, na hakuna karaha ndani yake. Kwa mujibu wa Hadithi ya Anas Ibn Malik, (R.A), amesema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Akilala mmoja wenu ukapita wakati wa Swala au ameisahau basi aiswali anapoikumbuka; Kwani Mwenyezi Mungu anasema: “Na ushike Swala kwa ajili ya kunikumbuka Mimi.” Imepokelewa kutoka kwa Imamu Muslim. Ujumla uliomo katika amri ya kuswali Swala zilizopita unaonesha kuwa inajuzu kuswali Swala zilizopita katika wakati wowote, hata katika nyakati za karaha. Huo ndio mtazamo wa wengi wa wanachuoni wa Fiqhi.

Share this:

Related Fatwas