Kulipa swala ndani ya wakati uliota...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kulipa swala ndani ya wakati uliotakatazwa

Question

Je Muislamu inafaa kulipa swala iliyompita ndani ya nyakati ambazo Sharia imekataza kuswali ndani ya wakati huo?

Answer

Kulipa swali zilizompita ndani ya nyakati zinazochukiza kuswali, Kisharia hakuna katazo, wala kuchukiza, kwa Hadithi ya Anas Ibn Maliki R.A amesema: Mtume S.A.W amesema:

“Pindi mmoja wenu akilala na kupitiwa na swala, au akaisahau, basi na aswali pale atakapokumbuka, kwani Mwenyezi Mungu Anasema: Simamisha swala kwa utajo wangu” Imapokewa na Imamu Muslimu.

Amri ya jumla iliyokuja ni mtu kulipa Swala zilizompita inaonesha kufaa kuzilipa wakati wowote mpaka ndani ya nyakati zinazochukiza kuswali, na haya ndio yaliyokubaliwa na Jamhuri ya Wanachuoni.

Share this:

Related Fatwas