Kukosa Swala ya Alfajiri kwa kulala...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kukosa Swala ya Alfajiri kwa kulala

Question

Ni ipi hukumu kukosa Swala ya Alfajiri kwa kulala?

Answer

Kunapendeza kisharia Muislamu kufanya haraka kutekeleza Swala mwanzo wa wakati wake, Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Abdullah bin Masoud R.A. amesema: nilimuuliza Mtume S.A.W.: ipi amali inayopendeza zaidi kwa Mwenyezi Mungu? Akasema: “Swala ndani ya wakati wake”. Ama kwa aliyekosa kutekeleza moja ya Swala ndani ya wakati wake kwa udhuru, kama kulala, kusahau au mfano wa hayo, basi kunapasa kwake kufanya haraka kuilipa Swala hiyo; Mtume S.A.W. amesema: “Mwenye kusahau Swala, basi kafara yake ni kuiswali atakapoikumbuka”. Mtu akiwa amelala akakosa Swala ya Alfajiri mpaka likachomoza jua, na hakukusudia kuikosa Saala hiyo, na hakuamka kwa kuwa amechoka sana, basi ni wajibu kwake kuilipa atakapoamka usingizini; Hadithi ya Safwan bin Muutil R.A. anasema: “….Hatukuwa tunaamka mpaka jua linachomoza”, akasema Mtume S.W.A : “Ukiamka Swali”.

Share this:

Related Fatwas