Wakati wa Swala ya Al-Duha na idadi ya Rakaa zake
Question
Ni upi wakati wa Swala ya Al-Duha? Na rakaa zake ni ngapi?
Answer
Wakati wa Swala ya Al-Duha huanzia baada ya jua kuchomoza mpaka kabla ya kupinduka (yaani kuanzia baada ya jua kuchomoza kwa dakika 20 mpaka wakati wa kabla ya Swala ya Adhuhuri kwa dakika 4), ama kuhusu idadi ya rakaa zake kwa uchache ni rakaa mbili, bora iswaliwe rakaa nne au zaidi; kwani Mtume (S.A.W.) alikuwa anaswali Swala ya Al-Duha rakaa nne na kuongeza kama anavyotaka.