Ufafanuzi wa Hadithi ya: Swala ndan...

Egypt's Dar Al-Ifta

Ufafanuzi wa Hadithi ya: Swala ndani ya wakati wake

Question

Nini maana ya Hadithi ya: Ibada bora zaidi ni swala ndani ya wakati wake?

Answer

Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Ibnu Masoud R.A. kwamba mtu mmoja alimuuliza Mtume S.A.W.: Ni ipi ibada bora zaidi? Akasema; “Sala ndani ya wakati wake, kuwatendea wema wazazi wawili kisha jihadi” Hadithi hii imepokolewa na Albukhary.

Hadithi hii si dalili ya kupasa Sala mwanzo wa wakati; kwa sababu neno “bora zaidi” linajulisha kwamba ibada zote mbili ni bora na moja yao inaizidi ubora nyingine, makusudio ni kwamba Sala mwanzo wa wakati wake ni bora zaidi ikiwa hakuna kinchozidi ubora huu, na hadithi imetaja Sala ndani ya wakati wake na haikubainisha kwamba ubora huu upo mwanzo wa wakati; Imamu Ibnu Daqiq amesema katika kitabu chake “Ihkamu Al-Ahkaam” (1/163): [Hakuna katika hadithi kinachoelezea mwanzo wa wakati na mwisho wake. Na makusudio yake: ni kuchunga isitoke nje ya wakati] Mwisho.

Share this:

Related Fatwas