Ughali wa mahari na athari zake
Question
Ni ipi hukumu ya Kisharia katika ughali wa mahari na athari zake?
Answer
Ughali wa mahari si katika mwenendo wa Uislamu, kwa sababu lengo asili la ndoa ni kumfanyia wepesi kijana wa kiiume na wa kike, kwani Mtume S.A.W anasema:
“Mwanamke mwenye baraka nyingi zaidi ni yule aliyeolewa kwa mahari nyepesi zaidi” imepokewa na Hakim.
Jambo la lazima ni kutofanya ugahali wa mahari, na baba anapaswa kurahisisha ndoa kwa watoto wake wa kike pindi anapopata kijana mwema wa kuoa ili kuwalinda vijana wa kiume na wa kike na vitendo vya ukiukaji, kwani Mtume S.A.W ametuletea nasaha tukufu kwa kauli yake:
“Pindi anapowajieni mtu munayemridhia dini yake na tabia zake basi muozesheni, na kama hamtafanya hivyo itakuwa ni fitina na uharibifu mkubwa duniani” imepokewa na Tirmidhiy.