Kumsalimia maiti kwenye kaburi lake...

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumsalimia maiti kwenye kaburi lake

Question

Je, mtu aliyekufa anahisi kwamba kuna mtu anamtembelea na kumsalimia?

Answer

Ndio, maiti anahisi mtu anayemtembelea na kumsalimia, na anamrudishia salamu, na anajisikia vizuri na anafurahia hilo, na hiyo ni kwa mujibu wa sheria za maisha ya Barzakh; Imepokelewa kutoka kwa Buraydah, (R.A), amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W), aliyekuwa akiwafundisha – yaani maswahaba watukufu- walipokuwa wakitoka kwenda makaburini, na msemaji wao husema: Salamu iwe juu yenu enyi watu wa majumba ya waumini na Waislamu, na sisi, Mwenyezi Mungu akipenda, tutakuwa wenye kufuata. Namuomba Mwenyezi Mungu atujaalie afya njema na kwa ajili yenu. "Imepokelewa kutoka kwa Imamu Muslim.

Imamu Ibn al-Qayyim katika “Al-Ruh” (uk. 5) anasema: [Mtume (S.A.W), alihalalisha kwa ajili ya umma wake, wanapowasalimia watu wa makaburini, kuwasalimia kwa maamkio ya wanao zungumza naye, basi husema: (Salamu iwe juu yenu enyi watu wa majumba ya waumini), na hii ni hotuba kwa anayesikia. Ni busara, na lau kuwa si hivyo, usemi huu ingekuwa katika hali sawa na hotuba ya asiyekuwapo na asiyekuwa na uhai, na waliotangulia wana kauli moja katika hili, na zimetajwa Hadithi kwamba maiti anajua kwamba aliyehai amemtembelea na kumfurahia.].

Na Mwenyezi Mungu ndiye anayejua zaidi

Share this:

Related Fatwas