Kumpa zaka mtu mwenye madeni

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumpa zaka mtu mwenye madeni

Question

Ni ipi hukumu ya kumpa zaka mtu mwenye madeni?

Answer

Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: “Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni wajibu ulio faridhiwa na Mwenyezi Mungu”[Al-Tawba, 60]. Aya hii imebainisha wanaopewa Zaka na ikataja miongoni mwao ni wenye madeni, ambao muda wa kulipa umefika na wakashindwa kuyalipa.

Kunajuzu kisharia kwa mwenye kutoa Zaka kumpa ndugu yake anayedaiwa ili alipe madeni yake, na katika hali kama hii kunakuwa na thawabu zaidi; kwa mujibu wa kauli ya Mtume S.A.W.: “Sadaka kumpa masikini ni sadaka ya kawaida, na kumpa ndugu inakuwa mambo mawili: sadaka na kuunga udugu”. Hadithi hii ameipokea Imamu Ahmad katika Musnad.

Na Mwenyezi Mungu ndiye Mjuzi zaidi.

Share this:

Related Fatwas