Kuheshimu watu wenye weledi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kuheshimu watu wenye weledi

Question

Je inapasa kuwarudia watu wa weledi katika mambo ya elimu na maarifa?

Answer

Mtume S.A.W ametufundisha kuheshimu weledi, pamoja na elimu ya Mtume S.A.W kutoka kwa Mwenyezi Mungu lakini alikuwa anatafuta ushauri kwa watu weledi miongoni mwa Maswahaba katika mambo yote ya kidunia ili kutufundisha kurudi kwa watu weledi, na Mtume S.A.W alikuwa akielezea weledi wa Maswahaba wake Watukufu ikiwa kuwapongeza, alisema:

 “Mtu mwenye huruma sana kwa Umma wangu ni Abubakiri, na mwenye nguvu zaidi katika dini ni Omar, mwingi wa haya ni Othman, mjuzi zaidi wa mambo ya faradhi ni Zaidi Ibn Thabiti, msomoji wao zaidi wa Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni Ubayy Ibn Kaab na mjuzi wao zaidi wa mambo halali na haramu ni Muadhi Ibn Jabal, fahamu kuwa katika kila Umma kuna muaminifu wao, na muaminifu zaidi wa Umma huu ni Ubaida Ibn Al-Jarrah”. Imepokewa na Imamu Ahmad, katika Hadithi hii kuna ufahamu kwa watu wawe na uelewa kuhusu huu weledi ili waweze kuutumia wanapokuwa na hitajio, au kuipa nguvu kauli ya mwenye weledi panopokuwa na mgongano.

Share this:

Related Fatwas