Haki za watu wenye umuhimu
Question
Je watu wenye umuhimu ni katika wanaostahiki zaka?
Answer
Mtu ambaye hana cha kukidhi mahitaji yake katika gharama zake au gharama za watu wake miongoni mwa chakula mavazi makazi matibabu elimu na mengine, inafaa kupewa mali ya Zaka mpaka kufikia kiwango cha kumtosheleza katika mahitaji hayo, na zingatio katika hilo ni hali ya mtu ikiwa huyo mtu ni katika makundi yaliyotajwa ndani ya kauli ya Mola Mtukufu:
{Kwa hakika wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni wajibu ulio uliowekwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hekima} At-Tawbah: 60.