Haki za Walemavu

Egypt's Dar Al-Ifta

Haki za Walemavu

Question

Ni nini haki za walemavu kwa mujibu wa sheria tukufu?

Answer

Kwa hakika sheria ya kiislamu ilitoa shime na uangalifu mkubwa kwa wenye ulemavu, ikawajibisha aina zote za kuwasaidia na kuwahimiza kupata elimu na kuwa na stadi mbalimbali za maisha, pamoja na kuwasaidia kugundua sifa na ubunifu wao, wakati huu huu ilikataza aina yoyote ya kuwadharau au kuwabagua, kwani sheria ya kiislamu ilikuja kwa kuwahimiza wanadamu wote washirikiana na kusaidiana, pamoja na kuchocheza tabia njema na kuepukana na maneno machafu na vitendo vibaya, kwa hiyo tunaona kuwa katazo la kuwajeli wengine na kuwabagua kwa majina au sifa liko wazi katika Qurani Takatifu, kama ilivyokuja katika kauli yake Mwenyezi Mungu: {Enyi mlio amini! Wanaume wasiwadharau wanaume wenzao, wala wanawake wasiwadharau wanawake wenzao. Huenda hao wakawa bora kuliko wao. Wala msivunjiane hishima, wala msiitane kwa majina ya kejeli. Ni uovu kutumia jina baya baada ya kwishaamini. Na wasio tubu, hao ndio wenye kudhulumu} [Al-Hujurat: 11] 

Share this:

Related Fatwas