Zaka ya Mapambo

Egypt's Dar Al-Ifta

Zaka ya Mapambo

Question

Ni Nini hukumu ya kisharia ya Zaka juu ya mapambo yanavyotumika kwa ajili ya kujiremba?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, Maswahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:

Wanachuoni wa Fiqhi wengi wanaona kuwa hakuna Zaka katika mapambo ya mwanamke, hata yawe kiasi gani, maadamu yanatumika kwa ajili ya kujipamba.

Na Imamu Al-Baihakiy amepokea kuwa Jabir ibn Abdullah aliulizwa kuhusu Zaka ya mapambo, Jabir akasema: Hakuna Zaka juu yake, na akasema: Hata vikifikia dinari elfu moja? Jabir akasema: nyingi sana”.

Kutokana na kile kilichotajwa, jibu la swali linajulikana.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Share this:

Related Fatwas