Maana ya Usimamizi

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya Usimamizi

Question

Usimamizi ni nini?

Answer

Jibu:

Mwenyezi Mungu Mtukufu akaweka uhusiano baina ya wanandoa kwa msingi wa mapenzi na huruma baina yao, Mwenyezi Mungu Mtukufu akasema: { Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri.} [Al-Rum: 21].

Nyakati fulani mambo hutokea ambapo familia inahitaji kufanya uamuzi hususa ambao una manufaa kwa washiriki wake. Kwa hiyo, Mwenyezi Mungu alimpa mwanamume katika suala hili haki ya kufanya uamuzi huo baada ya kushauriana na mke na wanafamilia wengine, na huu unaitwa usimamizi uliotajwa ndani ya Qur’ani Tukufu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: “Nao wanawake wanayo haki kwa Sharia kama ile haki iliyo juu yao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao.” [Al-Baqarah: 228], na Mwenyezi Mungu anasema: “Wanaume ni wasimamizi wa wanawake, kwa kufadhiliwa na Mwenyezi Mungu baadhi yao juu ya baadhi, na kwa mali yao wanayo yatoa.” (An-Nisaa:34)

Maana ya usimamizi ni kwamba mwanamume anamsimamia mke wake na familia yake kwa kumpa, kumlinda, kutunza na kukidhi mahitaji ya maisha familia kuhusu yale ambayo yanamnufaisha yeye na familia yake hivyo, ni wajibu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa mwanamume.

Share this:

Related Fatwas