Maana ya Al-Ashaaira.

Egypt's Dar Al-Ifta

Maana ya Al-Ashaaira.

Question

Ni wakina nani hao Al-Ashaaira, na ipi hukumu ya anayewaelezea kuwa wao ni Jahmiyah?

Answer

Mwanzo kabisa ni kuwa hawa Al-Ashaaira ni wale waliofuata Akida ya watu wa Salafu kama ilivyo, na wakasimamisha dalili na hoja mbalimbali ili kutetea Akida hiyo na kuinua bendera yake dhidi ya watu wa matamanio na makundi yaliyopotea yanayojinasibisha na Uislamu, au si Waislamu ni miongoni mwa wapagani ambao wanajadili juu ya Akida yao, kundi la Ashaaira lilifuata mfumo wa dalili za kiakili inayokusanya kati ya Andiko pamoja na akili, na wala hawakubali dalili ya kidhana katika kuthibitisha msingi wa Akida, madhehebu yao yalifuatwa na Jamhuri ya Wanachuoni Waislamu kwa kipindi kirefu, wao ni kundi kubwa la Umma na Akida yao ndio Akida ya Waislamu wa zamani na wasasa, wanamiliki Vyuo Vikuu vya Kiislamu kwa kutoa masoma mifumo na Akida. Al-Ashaaira ni watu wanaonasibishwa na Imamu Abil-Hassan Al-Ash’ary na kwa jina lake madhehebu yameitwa hivyo, Imamu Al-Ash’ary ameonesha wazi Akida ya waja wema waliotangulia kama ilivyokuwa kwenye zama za Mtume S.A.W. Maswahaba na Taabiin, na alifanya mijadala na makundi potofu na Mwenyezi Mungu kuyapa ushindi Madhehebu ya Watu wa Sunna (Ahlu Sunna), ikawa kama anavyosema Imamu Al-Murtadha Al-Zubaidy – Mungu amrehemu -  Pindi wanapoitwa Ahlu Sunna wal Jamaa basi kusudio lao ni watu wa madhehebu ya Al-Ashaaira na Al-Matrudiya, na huongezwa katika hilo kuwa Al-Ashaaira ni wale watu wa Imamu Abul Hassan Al-Ash’ary ambao walitokana na kundi la Muutazila na maneno yao ya misimamo mikali na upotoshaji wa mitazamo ya Wanachuoni wao, hivyo mwenye kupinga yeye mwenyewe kuwa kwake Ash’ary ni kana kwamba anasema kwa ulimi wake: “Mimi ni Muutazila”.

Ama mwenye kuwaelezea kuwa ni Jahmiya, huyo ni mjinga au mpotoshaji hana anachokijua kuhusu Akida ya Al-Ash’ariya.

Share this:

Related Fatwas