Dhana ya Hakimiya
Question
Ni nani wa kwanza kutumia dhana ya Hakimiya, na kwa namna gani dhana hiyo imeendelezwa katika fikra za kisasa?
Answer
Kwa hakika Al-Khawarij wa mwanzo waliojitokeza katika utawala wa Imamu Aly Ibn Abi Talib (R.A.) ndio wa kwanza kutumia dhana ya hakimiya, ambapo walidai kuwa Imamu aliridhika kwa hukumu za sahaba zake katika dini ya Mwenyezi Mungu, jambo ambalo ni kufuru, kwani hukumu ya pekee ni ya Mwenyezi Mungu wakatoa dalili kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Hapana hukumu ila ya Mwenyezi Mungu tu} [Yusuf: 40], lakini Imamu Aly aliwahoji kwa kusema: "Ni neno la haki lililotumika kwa ajili ya kuinusuru batili" [Imesimuliwa na Muslim], baadaye, dhana hii ilijitokeza upya kwa maana iliyoendelezwa na wakuu wa makundi ya kigaidi kama vile; Al-Mawdoody, Sayid Qutb chini ya istilahi ya Hukumu ya Mwenyezi Mungu au umoja wa hukumu, wakafanya umoja wa hukumu ni sehemu mojawapo sehemu za upweke wa Mwenyezi Mungu, ambapo ikikosekana itikadi na imani nzima huwa imekosa sehemu, mpaka kumhukumia Muislamu asiyeamini sehemu hii kuwa amekufuru na kutoka kwa Uislamu, nao walikusudia kwa sehemu hii kutekeleza Sheria za Mwenyezi Mungu, ambapo walidai kuwa katiba na kanuni zilizopo nchi za kiislamu ni kinyume na sheria kwani zimetungwa na watu, ilhali madhehebu za Kifiqhi na kanuni za kutungwa zote zimetungwa na watu, na kanuni ni mfumo au umbo lililoendelezwa kwa kutegemea hukumu za Kifiqhi.