Dhana ya Ujahili / Jahiliya

Egypt's Dar Al-Ifta

Dhana ya Ujahili / Jahiliya

Question

Ni nini dhana ya Jahiliya katika Qur`ani na Sunna, na kwa namna gani makundi ya kigaidi yametumia dhana hiyo kukufurisha jamii?

Answer

Dhana ya Jahiliya katika Qur`ani Takatifu na Sunna za Mtume huashiria kile kipindi kilichokuwa kabla Mtume Mohammed (S.A.W.) kutumwa na kupewa ujumbe, ni kipindi ambacho desturi za kishirikina na upagani zilienea kwa kuhalalisha yaliyo haramu, jambao ambalo halikuwa la waarabu hasa, bali jamii mbalimbali za zama hizo za kabla ya ujumbe wa Mtume (S.A.W.) Mwenyezi Mungu Amesema: "Na kaeni majumbani kwenu, wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya kizamani" [Al-Ahzab: 33], kwa maana ya kwamba: enyi wanawake msifanye kama walivyokuwa wakifanya wanawake wa zamani walioishi zama za kabla ya ujio wa Uislamu, iko wazi kuwa kipindi hicho kilimalizika kwa kutumwa kwa Mtume (S.A.W.) na kuteremshwa kwa Wahyi, na kwamba kufanya maovu na madhambi makubwa si sababu ya kutosha ya kumhukumu mtu kwa ukafiri, lakini makundi ya kigaidi yamegeuza matumizi ya dhana hii katika zama za kisasa wakaitumia vibaya kwa kuwakufurisha Waislamu pasipo na haki, wakidai kuwa jamii za kisasa zilirejea hali ya zamani katika enzi ya Kijahiliya ingawa wanakiri kuwa hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Mtume Mohammed ndiye mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na kusimamisha Swala, lakini ukweli ni kuwa makundi haya yamechafua dhana hii wakaibana kwa kuwakufurisha watu wakiichanganya na sheria kinyume na haki kwa kusudio la kujidai haki na Uislamu ilhali wao ndio wanaochafua dini na Waislamu.

Share this:

Related Fatwas