Dhana ya nchi katika Uislamu

Egypt's Dar Al-Ifta

Dhana ya nchi katika Uislamu

Question

Ni nini dhana ya nchi katika Uislamu? Na kwa namna gani makundi ya kigaidi yaligeuka mbali na dhana hii wakaitumia Kundi au Jama'a badala yake?

Answer

Nchi katika Uislamu hujengewa misingi mitatu; kwanza: ardhi, nayo ni eneo maalumu la kijiografia, pili: taifa nao ni wakaazi wa eneo lile la kijiografia, baadhi ya wataalamu wa Fiqhi waliongeza sharti kuwa wengi wa wakaazi wawe Waislamu tu, tatu: mfumo ambayo ni jumla ya kanuni na misingi ambayo hupanga mahusiano ya mtawala na raia na kwa upande mmoja na uhusiano wa raia wenyewe kwa wenyewe, nchi kwa nchi nyinginezo, katika nchi yoyote ya kiislamu kanuni hizo zinatokana na hukumu wazi za sheria ambazo huelezwa katika katiba kwa jina la misingi ya sheria.

Kinyume na hayo, makundi ya kigaidi ni mikusanyo ya watu wanao mielekeo ya kisiasa iliyojengewa vurugu pamoja na mikusanyo mingine katika jamii, ambapo magaidi wanaona kuwa nchi za Kimagharibi, Kiarabu na Kiislamu kwa mifumo yake, watawala wake na mataifa yake, ambapo fikra za makundi haya hushughulikia namna ya kubadilisha hali halisi kwa kutumia ukatili, kisha hudai kwa uongo kuwa wao ndio wanafuata njia ya Mtume (S.A.W.) na njia ya watu wema, hivyo, huwa inafanana na seli za saratani mwilini.

Share this:

Related Fatwas