Swala ya Haja

Egypt's Dar Al-Ifta

Swala ya Haja

Question

Ni ipi swala ya haja, hukumu yake na namna yake? 

Answer

Swala ya haja ni Sunna, na huswaliwa rakaa mbili katika rakaa hizo husomwa Suratul-Fatha na Aya chache zengine za Qurani, kisha husifiwa Mwenyezi Mungu na kuswaliwa Mtume S.A.W kisha kuomba duwa iliyopokewa katika Sunna.

Swala ya haja huswaliwa ili kuomba haja, na jamhuri ya Wanachuoni wanasema ni Sunna, na huswaliwa rakaa mbili mwenye kuswali katika kila rakaa husoma Suratul- Fatha na Aya chache za Qurani baada ya kusoma Suratul Fatha, kisha baada ya hapo hufuatiwa na wasifu kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kumswalia Mtume S.A.W kisha atamuomba Mwenyezi Mungu kwa duwa hii iliyopokewa kutoka kwa Mtume S.A.W:

“Mtu mwenye haja kwa Mwenyezi Mungu au kwa mwanadamu basi na atawadhe vizuri kisha aswali rakaa mbili kisha amsifie Mwenyezi Mungu na kumswalia Mtume S.A.W kisha na asema: Laailaaha illa Allah Al-Haliimu Al-Kariim, Subhaana Allah Rabbi Al-Arshi Al-Adhiim, Al-Hamdulillah Rabbil-Aalamiin, As-aluka muujibaat rahmatika wa azaaimu maghfiratika, walghaniimati min kulli birrin wassalaamati min kulli ithmi, Allahumma laa tadii dhamban illa ghafartah wala hamman illaa farrajtah wala haajatan hiya laka ridhaa illa qadhaitaha ya Arhamu Raahimiin” Imepokewa na Tirmidhy na Ibn Maja.

Hadithi hii imetaja idadi ya rakaa zake na namna ya kuiswali pamoja na duwa ambayo husomwa ndani ya swala hiyo.

Share this:

Related Fatwas