Swala ya kutaka ushauri.

Egypt's Dar Al-Ifta

Swala ya kutaka ushauri.

Question

Je swala ya kutaka ushauri inafaa kuswali ndani ya wakati wa kuchukiza?

Answer

Inachukiza Swala ya kutaka ushauri kuswaliwa ndani ya wakati unaochukiza kuiswali, nazo ni nyakati tano hatakiwi mtu kuswali ndani ya nyakati hizo isipokuwa kwa Swala yenye sababu: Wakati baada ya Swala ya Alfajiri mpaka kuchomoza jua, wakati wa kuchomoza kwa jua mpaka likamilike na kupanda kidogo kwa kiasi cha urefu wa mkuki, nayo ni wastani wa dikika ishirini baada ya kuchomoza, jua linapokuwa kati kati mpaka lisogee kidogo, kwa kiasi cha muda wa dakika nne kabla ya adhana ya Adhuhuri, na baada ya Swala ya Alasiri mpaka kuzama jua, na wakati wa kuzama kwa jua mpaka likamilike kuzama kwake, na hiyo ni kauli za Jamhuri ya Wanafiqhi wa Madhehebu ya Abu Hanifa, Maliki na Imamu Shafi, ikiwa mtu ataiswali inafaa kuiswali pamoja na kuchukiza, na inafaa bila kuchukiza kwa Madhahebu ya Imamu Hambali.

Share this:

Related Fatwas