Masharti ya ulinganiaji

Egypt's Dar Al-Ifta

Masharti ya ulinganiaji

Question

Ni yapi masharti yanayohitajika kupatikana kwa anayeshughulikia ulinganiaji katika Uislamu?

Answer

Mlinganiaji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu hupaswa kufuata njia ya hekima na upole katika kazi yake, Mwenyezi Mungu Anamsifu Mtume (S.A.W.) na mtindo wake wa kuwalingania watu katika Uislamu Akisema: "Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata" [Yusufu: 108], kwa hiyo mlinganiaji anapaswa kutambua malengo ya Sharia na hatima za mambo akiwa na ujuzi wa kutosha kuhusu changamoto za jamii yake, pia, awe na maarifa ya taaluma mbalimbali za kisharia na kiarabu akijihusisha na fani mojawapo fani za taaluma hizo ili awe na ujuzi na elimu, pia, awe na imani akiwa anajitahidi katika kutekeleza majukumu ya ulinganiaji kwa ajili ya Mwenyezi Mungu bila ya kujali mapato ya dunia wala matamanio binafsi, Mwenyezi Mungu Amesema: "Nao hawakuamrishwa kitu ila wamuabudu Mwenyezi Mungu kwa kumtakasia Dini" [Al-Bayyinah: 5], naye Mtume (S.A.W.) alisema: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu hakubali kazi isipokuwa iliyofanywa kwa ajili yake tu" (Imesimuliwa na Al-Nasaiy), aidha, miongoni mwa masharti muhimu ya mlinganiaji awe mfano wa kuigwa akiwajibika mafunzo anayoyaeneza na kuelekeza watu kuyafanya kati ya vitendo, maneno na miamala, awe mjuzi wa hali halisi ya jamii yake hasa mila na desturi za watu na hali zao, asiwazungumzie kwa mtindo wasioufahamu akawa  ni sababu ya kukufuru kwa watu hawa na kumkadhibisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake, kwa kweli mlinganiaji bora zaidi ni Mtume (S.A.W.) ndiye mfano wa kuigwa kwa wote kwa hivyo Mwenyezi Mungu Amemsifu: "Hakika nyinyi mnayo ruwaza njema kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu" [Al-Ahzaab: 21], tabia zake (S.A.W.) zilikuwa zinatokana na Qur`ani, naye ndiye Imamu wa walinganiaji kwa Mwenyezi Mungu (S.W.) 

Share this:

Related Fatwas