Mashambulizi ya kujitolea / kujiua

Egypt's Dar Al-Ifta

Mashambulizi ya kujitolea / kujiua

Question

Je, Ni ipi hukumu ya mashambulizi ya kujitolea au ya kujiua yanayotekelezwa na makundi ya kigaidi? 

Answer

Ni wazi kwamba mashambulizi ya kujitolea yanayotekelezwa na makundi ya kigaidi kulenga wasio na hatia kutoka tabaka na makundi mbalimbali ya jamii, pia mtazamo wa makundi haya ya kigaidi kwa wanaokataa fikra zao potofu na kuwatuhumu ukafiri na kuwahukumu kifo ni mtazamo finyu ambao hauwakilishi dini ya kiisalmu wala sharia yake iliyosisitiza kuimarisha amani, utulivu na uslama kwa dunia nzima.

Sharia ya kiislamu imekataza umwagaji damu kwa ujumla, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {aliye muuwa mtu bila ya yeye kuua, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewaua watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote} [Al-Maidah: 32], kwa hizo jinai zinazofanywa na makundi ya kigaidi haziafikiani na sharia ya kiislamu na malengo yake makuu likiwemo lengo la kuhifadhi nafsi ya kibinadamu na kuiheshimu, isitoshe, bali jinai hizo huchafua taswira ya Uislamu na Waislamu kwa kuituhumu dini hiyo kwa kuhusika kwa mauaji na umwagaji damu pasipo na haki.

Hivyo, mashambulizi haya hayajuzu katika Uislamu.

Share this:

Related Fatwas