Fadhila za kutoa vyakula
Question
Ni nini fadhila za kutoa vyakula katika Uislamu
Answer
Matini kadha wa kadha zilinukuliwa katika Qurani na Sunnah za Mtume za kuthibitisha kuwa kuwalisha watu ni mojawapo amali bora kwa Mwenyezi Mungu (S.W.) na ni karibu zaidi kukubaliwa na Mwenyezi Mungu (S.W.) mpaka ikawa sababu mojawapo sababu za kuingia peponi, Akisifu waja wake waumini, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake} [Al-Insan: 8], na kutoka kwa Abdullah bin Amr (R.A.) kwamba mtu mmoja alimwuliza Mtume (S.A.W.): “ni nini iliyo bora katika Uislamu? Akasema Mtume: kulisha chakula, kutoa salamu kwa uanyemjua na usiyemjua” imekubaliwa na wote. Na kutoka kwa Ali bin Abi Talib (R.A.) kuwa alisema: Mtume (S.A.W.) alisema: “Peponi kuna vyumba vya hali ya kuwa kilicho chini yake huonekana kwa aliye juu, na kilicho juu huonekana kwa aliye chini” akasimama mwarabu mmoja akasema: ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu ni kwa nani hasa? Akasema Mtume: “ni kwa mwenye: kusema maneno mema, kulisha chakula, kufunga mara kwa mara, kusali usiku ilhali watu wamo usingizini” imesimuliwa na Ahmed.