Faida za kibenki
Question
Ni zipi sababu za kusema kuwa kunajuzu kufaidika na faida za kibenki
Answer
Ofisi ya Mufti wa Misri, imeeleza kuwa: kunajuzu kufaidika na faida za kibenki kwa kuzingatiwa ni faida za ufadhili zinazotokana na mikataba inayofikia maslahi ya pande zake; na hii kwa sababu kadhaa:
Kwanza: kwamba kanuni inasema: kunajuzu kuendelea mkataba mpya ikiwa Hauna udanganyifu au madhara, na mikataba ya benki ni ya aina hii.
Pili: kwamba masuala haya kumedhihiri ndani yake kwamba maslahi ya uma ni ya nchi na Maslahi binafsi ni ya watu wenyewe katika kuendesha miamala na kunufaika na shughuli za kibenki kwa sababu huu ni mwamvuli wa kiuchumi ambao unadhibiti soko la fedha, na viwango vya mfumuko wa bei, na kuongezeka kwa haraka viwango vya maendeleo kwa kufadhili shughuli zote za kiviwanda, biashara na nyinginezo.
Tatu na mwisho: kwamba kanuni za kibenki za Misri namba 88 ya mwaka 2003, na Sheria yake ndogo ya kiutendaji iliyotoka 2004, zimeeleza kwamba mahusiano kati ya mteja na benkini mahusiano ya kiuwekezaji na ufadhili, na si mkopo.
Nahii ndio Fatwa ya zama na zama.