Bima ya Magari
Question
Je, inaruhusiwa kisharia kuweka bima ya jumla ya magari ya kubeba mizigo kwa lengo la kupata fidia ya kifedha kwa mwenye gari likipatwa na ajali au moto au wizi?
Answer
Bima ya magari inajuzu kwa jumla, ambapo huwa sawa sawa na kutoa msaada wakati wa msiba au shida yaani ni aina ya kusaidiana, kwani ni mchango wa kweli na siyo fidia, na ni sura mojawapo za kusaidiana na ushirikiano katika wema ulioagizwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu: {Na saidianeni katika wema na uchamungu} [Al-Maidah: 2]