Israa na Miraji
Question
Ni nini matukio yaliyotukia katika safari ya Israa na Miraji?
Answer
Mtume (S.A.W.) alisafiri akiwa macho kutoka Msikiti Mtukufu kwenda Msikiti wa Al-Aqsa akasali imamu na nyuma yake walisali Malaika na Mitume (A.S.), kisha alipanda mbinguni kutoka Msikiti wa Al-Aqsa kwenda Mkunazi wa mwisho, ambapo katika usiku huu Mtume (S.A.W.) aliona pepo akaangalia malipo na makazi mema Aliyoyaandaa Mwenyezi Mungu kwa waumini wachamungu, wakati huo huo Mtume (S.A.W.) aliona moto akaangalia adhabu na mateso yaliyoandaliwa kwa makafiri na washirikina, na akaona miujiza kadhaa mikubwa mikubwa kama vile taswira ya Malaika Jibrili akiwa na mabawa (600), pamoja na Mkunzi wa mwisho ukiwa na mambo ya ajabu mengi ya Mwenyezi Mungu (S.W.) akamwona Mola wake Mlezi kwa macho yake, bila ya alama wala miale ya mwanga inayounganisha (S.W.) na kuzungumza na Mola wake (S.W.) pasipo na kiunganishi wala pazia: Mwenyezi Mungu Amesema: {Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alichomfunulia* Moyo haukusema uwongo uliyo yaona} [An-Najm: 10-11].
Katika usiku huo, Mwenyezi Mungu (S.W.) Alifaradhisha juu ya Mtume wake (S.A.W.) na umma wake kusali sala tano kila siku, ambapo malipo ya sala moja ni sawa na sala kumi; maana sala tano zina malipo ya sala hamsini kwa siku, Akamhusisha Mtume wake kwa sifa na vyeo vya juu kabisa kuliko Mitume na Manabii wenzake wote (A.S.) hiyo ndiyo rai ya jamaa ya maulamaa wa hadithi, fiqhi na mantiki, pia matini za sheria ziliyaunga mkono maoni haya.