Sanaa ya uchoraji.

Egypt's Dar Al-Ifta

Sanaa ya uchoraji.

Question

Nini hukumu ya kuchora baadhi ya picha kwenye nguo au kutani au sehemu zingine?

Answer

Hakuna ubaya mfano wa picha kama hizo na michoro, madamu hizo picha hazina mambo yasiyofaa kuoneshwa au kuchorwa, kama picha za uchi au kitendo kisichofaa, au kuchochea ukiukaji wa amri za Sharia, au kutoka kwenye kumtii kiongozi mkuu wa nchi (sheria au kiongozi au nchi) ikiwa picha hizo zitakuwa na mambo kama hayo ni haramu hizo picha, sio tu kwa kuwa ni picha, bali ni kwa jambo lililonje ya usahihi wake, nalo maudhui yake inakusanya sanaa iliyozuiliwa, yanayosisitiza uhalali wa picha za kuchora juu ya majengo na zinazofanana na hizo, ni Hadithi iliyopokelewa na Abi Twalha R.A kuwa Mtume S.A.W amesema:

 “Malaika hawaingii kwenye nyumba yenye picha”. Amesema Busra: Zaidi Ibn Khalib aliumwa tukamtembelea, tukiwa ndani ya nyumba yake tukaona pazia likiwa na michoro ya picha, nikamuuliza Abdillah Al-Khaulany:  Hivi hajatuambia kuhusu picha? Akasema: Ndio alisema: Isipokuwa kwenye nguo, hivi hukumsikia? Nikasema: Hapana, akasema: Hapana alisema.

Share this:

Related Fatwas