Viwango vya ukafiri

Egypt's Dar Al-Ifta

Viwango vya ukafiri

Question

Je, ukafiri na viwango, sehemu kufuatana na tofauti za hukumu?

Answer

Ukafiri ni kukana na kukataa mambo yaliyopitishwa katika dini ya Bwana wetu Mtume Mohammed (S.A.W.) kama vile; kukana uwepo wa Muumbaji wa ulimwengu, Unabii wa Mtume (S.A.W.), kukana ibada zilizofaradhishwa katika dini na nguzo za dini, kuhalalisha yaliyo haramu kwa dalili thabiti n.k., pia, ukafiri hurejelea kukana mema na mazuri.

Ukafiri unao viwango ambapo kuna ukafiri ambao humsababisha mtu kutoka katika dini, na aina nyingine ambayo anayepatwa nayo hahukumiwi kuwa ametoka katika dini, bali huitwa mhalifu au mwasi.

Ukafiri unao viwango vinne: Ukafiri wa kukana, ukafiri wa kutotambua, ukafiri wa kukataa na ukafiri wa unafiki kwa mujibu wa aliyoyasema Al-Azhary, pia, ipo aina ya ukafiri kwa kisicho Mwenyezi Mungu nao ni ukafiri ulio katika kiwango cha chini maana ni aina nyingine mbali na ukafiri kwa Mwenyezi Mungu, aina ya kwanza husababisha kutoka katika dini na kustahiki adhabu ya milele motoni, na ya pili husababisha ubaya tu pasipo na kutupwa motoni kwa milele.

Mifano: Kuwepo mtu anayeamini upweke na Unabii kwa ulimi na moyo wake, lakini wakati huo huo anafanya madhambi makubwa makubwa kama vile; mauaji, kuharibu nchi, kupoteza haki za wengine, kukana neema za Mwenyezi Mungu n.k, kwa kuelezea hayo zipo Hadithi za Mtume (S.A.W.) ambazo zimesawazisha madhambi makubwa na ukafiri kama vile kauli yake Mtume (S.A.W.): "na kupigana naye (Muislamu) ni ukafiri" imekubaliwa na wote, na kauli yake katika kuelezea hali na hatima ya anayeacha Swala kimakusudi: "Yeyote atakayeacha Swala kwa makusudi basi huwa amekuwa kafiri" imesimuliwa na Al-Tabarany katika kitabu chake cha Al-Awsat na mifano mingine mingi, ambapo japokuwa matini imetumia neno kafiri lakini maana lengwa ni ubaya ua dhambi, au hata ni aina ya ukafiri ulio chini ya ukafiri ulio wazi, kwa hiyo Khawariji hawatokuwa na pingamizi kuhusu hukumu ya anayefanya madhambi makubwa makubwa kuwa kafiri pia.

Hakuna Muislamu hata mmoja zamani na sasa anayesema kuwa madhambi husababisha mtu awe ametoka katika dini, kinyume na Khawariji ambao wanaona kuwa kufanya madhambi makubwa ni sababu ya kutosha ya kumhukumu mtu kafiri.

Share this:

Related Fatwas