Athari za uvumi kwenye jamii

Egypt's Dar Al-Ifta

Athari za uvumi kwenye jamii

Question

Upi wajibu wa Muislamu kuhusu yanayoibuka pembezoni mwake miongoni mwa maneno ya uzushi.

Answer

Uislamu umekausha vyanzo vya uzushi kwa kuwapa amri Waislamu kufanya uchunguzi wa habari kabla ya kuleta hukumu, na ukaamrisha mambo kurudishwa kwa wahusika wake na kulijua vizuri kabla ya kuanza kulisambaza na kulizungumzia, Mola Mtukufu Amesema:

{Enyi mlio amini! Akikujieni mpotovu na habari yeyote, ichunguzeni, msije mkawasibu watu kwa kutojua, na mkawa tena wenye kujuta kwa mliyo yatenda} Al-Hujrat: 6.

Kama vile umekataza kusikiliza uzushi na kuueneza, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewalaumu ambao wanawasikilizisha watu uzushi na fitina, Mola Mtukufu Amesema:.

{Lau wangeli toka nanyi wasingeli kuzidishieni ila mchafuko, na wange tanga tanga kati yenu kukutilieni fitna. Na miongoni mwenu wapo wanao wasikiliza. Na Mwenyezi Mungu anawajua madhalimu} Attawba: 47.

Share this:

Related Fatwas