Ukweli wa makundi ya kigaidi

Egypt's Dar Al-Ifta

Ukweli wa makundi ya kigaidi

Question

Namna gani Wanachuoni wa Uislamu wanaona ukweli wa makudni ya kigaidi yenye misimamo mikali?

Answer

Makundi yote ya kigaidi yanakubaliana kukusanya kati ya ujinga katika dini ya Mwenyezi Mungu na kati ya uthubutu wa kukufurisha Waislamu na kuhalalisha damu zao, na kudhulumu waja wa Mwenyezi Mungu, jambo linalopelekea kusema kuwa hayo makundi ni chombo mikononi mwa maadui wanayatumia katika kuelekeza mishale yao kwenye moyo wa Umma, hilo ni kwa sababu mfumo wa makundi haya ya ukufurisshaji wa kigaidi unapelekea kuongeza tofauti na migawanyiko na kukuza uadui na chuki kati ya Waislamu, kama vile unapalekea kuvunja misingi ya Uislamu na kuchafua sura yake jambo linalotoa nafasi kwa maadui wa Uislamu kupata mwanya wa kushambulia Uislamu wakati ambapo Waislamu wapo salama.

Makundi hayo ya kigaidi tokea kuanzishwa kwake yamekusudia kueneza hali ya wasi wasi kati ya watu kwa njia yenye kuleta fitina na kwa sura ya kuvunja moyo, lengo ni kuonesha nguvu yake na kufikisha ujumbe wake kwa sehemu kubwa ya watu kwa ajili ya kuwatisha na kuwahofisha kupambana nao, kuongezea pia kufanya kazi ya kuleta wafuasi wapya wale wenye nafsi za kukiuka ambazo zinaelekea kwenye vitendo vya matumizi ya nguvu ili kusaidiwa kwenye uwanja wa vita ambavyo wanaviendesha, kama vile makundi haya yanafanya mauaji ya watu wengi wasiowakubali. 

Share this:

Related Fatwas