Mawazo ya makundi ya kigaidi.

Egypt's Dar Al-Ifta

Mawazo ya makundi ya kigaidi.

Question

Ni yepi mawazo muhimu ya kijihadi kwa makundi ya msimamo mkali?

Answer

Makundi yote ya kigaidi yanafanya kazi ya kuleta hotuba za kidini za aina moja kupitia kuwaahidi wafuasi kuingia Peponi walizoahidiwa wakati watakapo kufa kama mashahidi wakiwa kwenye makundi hayo na si mengine, nayo ni Jihadi maalumu kwao tu ambayo inavuta idadi kubwa ya wale waliokosa hisia au uzalendo miongoni mwa vijana wenye umri mdogo ambao wanapenda mambo ya hatari katika wigo wa Kiislamu bila ya kufahamu wala kuwa na mtazamo.

Ukweli ni kuwa Jihadi hii inachukua nafasi kubwa katika kujitangaza makundi yote na mitandao ya msimamo mkali kwa kipindi kirefu, nayo inachukua nafasi ya hamasa kubwa ambapo nafasi ya kupenda kufa shahidi na kuingia Peponi, katika kundi la Hashashiin Hassan Sabah ametengeneza pepo ndani yake kuna mabustani mito pombe na wanawake wakiimba na kucheza kana kwamba wao ni wanawake wa Peponi “Huuru Al-Ain”, na tunakuta mtandao wa “isis” wanatangaza fikra hii pia kwani ameonekana mmoja wa watu wa mtandao katika moja ya video akisisitiza kuwa yeye ameona wanawake wa peponi, akisifu uzuri wa uke wa wanawake wa peponi baada ya kujeruhiwa katika moja ya vita, ambapo anasema ameona pepo ndani yake kuna wanawake wazuri sana, kama vile anasisitiza kuwa amemwona Mtume wa Mwenyezi Mungu na akamtaka abakie katika dola ya Kiislamu kwani ni haki. 

Share this:

Related Fatwas