Mtazamo wa makundi ya kigaidi wa ma...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mtazamo wa makundi ya kigaidi wa matukio

Question

Je makundi ya kigaidi yanaruhusu wafuasi wao kuwa na uhuru wa kufikiri na kutafiti matukio?

Answer

Makundi ya kigaidi yanategemea kupotosha akili za wafuasi wao na kuondoa ufahamu wao ili wawe chombo cha utiifu kwa kiongozi wao na amiri wao, ambapo anawaamrisha na wanateeleza mpaka kufikia kiwango cha kujiua wao wenyewe bila ya  kujiuliza, katika kundi la “isis” tunakuta wanaosimamia kundi wanatumia njia za kiteknolojia za kisasa na mitando ya mawasiliano ya kijamii ili kuibua kwa wafuasi wao hisia kali na kuvuta wafuasi wengine wapya kwenye safu zao ambapo mitando hii ya mawasiliano ya kijamii imekuwa na nafasi muhimu sana katika kueneza fikra za kigaidi, ambapo huonekana sura iliyopo kwenye mitandao hii kuwa inaleta tiba ya hali za wasi wasi kwa wafuasi wapya kwa mambo yasiyofahamika, kwa mfano kuna wapiganaji wengi wanasambaza picha zao wakiwa na paka pamoja na wanyama, pamoja na kuwa kuna video nyingi zinaonesha wapiganaji wa makundi hayo na baadhi yao wakiwa si Waarabu wakifanya vitendo vya kutisha ikiwa ni pamoja na mauaji na ukandamizaji, sura ya jumla ambayo wanaionesha wapiganaji wa “isis” kuhusu maisha yao zinaleta urafiki wa karibu na roho nzuri na harakati zenye malengo, na wote wamekuwa na hisia za ushujaa wa uongo, uliotengenezwa ili kuleta wafuasi wengi na wapiganaji.

Share this:

Related Fatwas