Mtazamo wa makundi ya kigaidi kwa b...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mtazamo wa makundi ya kigaidi kwa baadhi ya masuala ya Umma

Question

Ni namna gani watu wa fikra za kigaidi wanazungumzia masuala muhimu ya Umma, kama vile suala la mwanamke, Sanaa, Sheria za sasa na mengine miongoni mwa masuala yaliyosambaa?

Answer

Watu wa makundi haya wanamfanyia uadui mwanamke na wanawaharamishia kutoka majumbani isipokuwa kwa dharura, kisha suala la kusoma na kufanya kazi si katika mahitaji ambayo yanapelekea mwanamke kutoka, hivyo kumzuia mwanamke kufanya kazi. huo ni uadui kwa mahitaji yake anayoyahitaji, kwani kumzuia kusoma na kupata elimu kunazingatiwa ni uadui wa kijinga kwa mahitaji anayoyahitaji hivi sasa na hapo baadaye.

Kama wanavyona watu wa kukufurisha kuwa dola ya Kislamu ndio ambayo inazuia mambo ya kuimba na mziki pamoja na mambo ya sanaa na michezo, wala hazitambui mabenki ya biashara na masoko ya hisa pamoja na mikopo, nazo pia ndio zinajenga mfumo wa kielimu unalea watoto wake kwenye ustaarabu wa sasa pamoja  na mitindo ya maisha iliyopo duniani, na kufuata mtindo wa maisha ya waja wema waliotangulia, kama wanavyoona pia ndio dola ambayo inazingatia upigaji picha na kuchapa karatasi pamoja na michoro ni haramu kisharia, na kutahadharisha na kushirikiana na kila yanayohusiana picha pamoja na upigaji picha, mfano maduka vifaa na vyombo vya kupigia picha na vya uchoraji pamoja na runinga sinema na mambo mengine.

Kama wanavyoona kuwa dola ya Kiislamu ndio ambayo inatahadharisha kushirkiana na mashirika taasisi mabenki na maduka ya kubadilisha pesa na kutumia sheria za kutungwa zenye kuitwa za kitaifa na kimataifa kwa sababu ya kupingana kwake na hukumu za Mwenyezi Mungu, kama vile wanazuia mashirikiano yeyote ya kifedha wanayoona yanariba ndani ya majimbo ya Kiislamu au na nchi za kikafiri, ambapo hilo linazingatiwa kwenda kinyume na mafunzo ya Kiislamu. 

Share this:

Related Fatwas