Makundi ya kigaidi yako mbali na ha...

Egypt's Dar Al-Ifta

Makundi ya kigaidi yako mbali na hali halisi

Question

Ni nini sababu ya kwamba makundi ya kigaidi yanajiweka mbali na hali halisi ya mambo ya jamii, kuhusiana na namna ya mavazi au mfumo wa maisha ya kila siku au fikra?

Answer

Kwa hakika, makundi ya kigaidi na wanaowaunga mkono wanashikilia mbinu iitwayo: "Kufananisha hali kwa matini" au kwa jina jingine: "Qadari zilizo fanana" kwa maana ya kufananisha hali halisi kwa yaliyokuja katika matini ya Qur`ani Tukufu kupitia kudai kuwa kundi lililopo katika hali halisi ni hilo hilo linalolengwa na matini ya Qur`ani bila ya kujali kuwa hukumu ni sawa sawa au la.

Tatizo la suala hilo ni kuwa makundi ya kigaidi yanategemea matini ambazo zimeteremka katika muktadha maalumu au matukio binafsi katika historia, na kwamba kuzitumia matini hizi kwa muktadha mwingine wakidhani kuwa wao ndio wanaolengwa na matini, mifano ya hayo ni mingi kama vile; matini zilizokuja kwa ajili ya kufafanua mambo ya ghaibu yaliyotajwa na Mtume (S.A.W.) kwa uwezo aliopewa na Mwenyezi Mungu kwa fadhila ya Unabii.

Kwa mfano; bendera nyeusi zimejitokeza katika ulimwengu wa kiislamu kwa kuwa wabebaji wake wanajifanya wao ndio waliokusudiwa na kauli yake Mtume (S.A.W.): "Mkiona wabeba bendera nyeusi wakija kwa upande wa Khurasan, basi jiungeni nao kwani miongoni mwao Khalifa wa Mwenyezi Mungu Al-Mahdy".

Magaidi wakajaribu kujifananisha na waliotajwa katika Hadithi wakajitokeza wakibeba bendera nyeusi ili wawakusanye watu nyuma yao wakidai kuwa wao ndio waliokusudiwa na Mtume katika Hadithi. Hivyo ndivyo, kwa kupita wakati na zama yanajitokeza makundi na jamaa wanaobeba bendera hizo wakidhani kuwa wanatekeleza yaliyokuja katika Hadithi hii na dalili nyinginezo.

Katika zama hii, tunaona baadhi ya wafuasi wa makundi ya kigaidi wakidai kuwa wanatekeleza mafunzo yaliyomo ndani ya Hadithi za Mtume wakazifanya hukumu za sheria ambazo ni wajibu kutekelezwa.

Share this:

Related Fatwas