Vidhibiti vya kufungamanisha Hadith...

Egypt's Dar Al-Ifta

Vidhibiti vya kufungamanisha Hadithi za fitina na hali halisi

Question

Ni upi wajibu wa Muislamu kuhusiana na Hadithi za kuzungumzia hali ya siku za mwisho wa dunia, na kwa namna gani makundi ya kigaidi yalizifasiri Hadithi hizo?

Answer

Kwa hakika kusoma na kuchunguza Hadithi za kuzungumzia hali ya siku za mwisho wa dunia ni jambo linaloruhusiwa, bali kuyaamini yaliyokuja nayo Hadithi ni jambo la msingi katika imani ya Muislamu, ambapo Muislamu anatakiwa kuamini ghaibu kwa mujibu wa Qur`ani na Sunna sahihi, ama kufungamanisha zile Hadithi na matukio binafsi basi ni jambo linalotakiwa kuchunguzwa kwa undani, na dalili ya kuruhusu hukumu hii ni kuwepo mifano ya kufungamanisha Hadithi za fitina kwa matukio maalumu kama ilivyokuja katika Fiqhi ya watu wema wa umma.

Lakini kuhusisha Hadithi za fitina kwa matukio maalumu kunalazimika vidhibiti kama vile; kutoa hukumu hii baada ya tukio si kabla halijatokia, nalo ni sharti wazi lisilo na shaka kwa dalili ya kuwa Maswahaba wamefanya hivyo, ambapo Khuzaymah hakuliamini kundi dhalimu ila baada ya kuuawa kwa Ammar Bin Yasser (R.A.), naye Asmaa bint Abi Bakar hakutoa hukumu juu ya Al-Hajjaj na Al-Mukhtar Al-Thaqafy ila baada ya kutokea mauaji na uharibifu kutoka kwa Al-Hajjaj na uongo na kashfa kutoka kwa Al-Mukhtar.

Na kuhusisha Hadithi za suala fulani kwa mambo yasiyokusudiwa kumesababisha matatizo mengi kwa umma na kuchangia kuenea shari kubwa kwa kufasiri Hadithi za Mtume (S.A.W.) kimakosa, kama vile kuhusisha Hadithi za Al-Mahdy kwa mtu binafsi na kushikilia maoni maalumu, hivyo Waislamu kutofautiana sana mpaka kupigana na kuvunja heshima pasipo na sababu.  

Share this:

Related Fatwas