Duru ya akili katika kuelewa Qur`an...

Egypt's Dar Al-Ifta

Duru ya akili katika kuelewa Qur`ani na Hadithi na kutengeneza Minhaj sahihi

Question

Ni ipi duru ya akili katika kuelewa Qur`ani na Hadithi na kutengeneza Minhaj sahihi?

Answer

Akili ni chombo cha uelewa na kuchagua, nayo inaendana na maumbile, na kwa akili humpambanua mwanadamu na viumbe hai vingine, na akili sio ubongo uliopo kichwani na una mahusiano nao, Mwenyezi Mungu Anasema: (Je! Hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo zao za kuzingatia)[Al-Hajj, 46]. Na kwa akili Wanazuoni wa Kiislamu wamethibitisha kwa pamoja kwamba miongoni mwa mambo makubwa ambayo yamejengewa dini, kama ulazima wa kuwepo muumba katika ulimwengu huu, na ulazima wa kutakaswa na kuwa na mshirika, ulazima wa kusifika kwake na ukamilifu unaoendana na utukufu wake, na ni muhali kusifika kwake na upungufu wowote, na ulazima wa kusifika mitume yake na ukweli, uaminifu na uelevu. Na akili ina duru kubwa katika kutambua zuri na baya, akili inatambua uzuri wa ukweli na ukarimu, ubaya wa uongo na ubahili, hivyo basi ukweli unasifiwa na uongo unakosolewa na watu wenye akili katika zama na staarabu mbalimbali. Ama hukumu za Kifiqhi akili sio chanzo chake, lakini inazitoa na kuzifahamu kutokana na Matini za kisharia, na hilo ni katika kuangazia kanuni za kutoa hukumu ambazo zimeelezewa na Wanazuoni.

Share this:

Related Fatwas