Hukumu ya kutoa wasia kwa mmoja wa warithi aliye na ulemavu
Question
Ni ipi hukumu ya kutoa wasia kwa mmoja wa warithi aliye na ulemavu?
Answer
Hakuna pingamizi lolote la kisharia mtu atoe wasia kwa sehemu ya urithi wake kwa mmoja au zaidi ya warithi wake walio na ulemavu, bali huwa anastahiki malipo mema kwa wasia yake hiyo, kwa kuwa anawasaidia kupata cha kuwasaidia katika maisha yao badala ya kuomba msaada wa watu na kusubiri hisani zao.