Hukumu ya kuugusa msahafu ulioandikwa kwa mfumo wa Braille kwa asiye na udhuu
Question
Ni ipi hukumu ya asiye na udhuu kuugusa mshafu ulioandikwa kwa mfumo wa Braille kwa vipofu?
Answer
Muislamu anapaswa kuitukuza Qur`ani, kuiheshimu, kuitakasa na kuitunza vizuri. Na ni alama ya kuitukuza na kuitunza Qur`ani kutoguswa isipokuwa kwa aliye na udhuu, ambapo haijuzu kuguswa na aliyeharibu udhuu wake kwa kuwa na uchafu mkubwa au mdogo, msahafu ulioandikwa kwa mfumo wa Braille kwa vipofu huwa na hukumu hiyo hiyo ya msahafu wa kawaida, hivyo inapaswa kutunzwa, kuheshimiwa na kutukuzwa, na inakatazwa kuguswa na asiye na udhuu kulingana na kauli iliyopendekezwa kutokana na kauli za wanavyuoni.
Na atakayeona haraja au mashaka akahitaji kusoma Qur`ani kwa kutumia aina hii ya msahafu moja kwa moja kwa kutaka kukidhi dharura ya uhifadhi au kujifunza au ugumu wa kupata anayemsaidia kutia udhuu, basi anaruhusiwa kutumia msahafu ulioandikwa kwa mfumo huu, kwa mujibu wa walioruhusu hayo kutoka kwa wanafiqhi wa Madhehebu ya Malikiya.