Hukumu ya Kutumia Kipulizia Pumu (...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kutumia Kipulizia Pumu (Dawa ya Pumu) kwa mwenye Saumu

Question

Nini Hukumu ya matumizi ya Kipulizia pumu katika Saumu?

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata, na baada ya hayo:

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameifaradhisha Saumu kwa waja wake Waumini na akaijaalia kuwa ni moja ya Nguzo tano za Uislamu ambazo haukamiliki Uislamu wa mtu isipokuwa kwazo, ameipwekesha kwa mipaka ambayo atakayeivuka atakuwa ameivuruga Saumu yake au itapungua kwa mujibu wa kitendo alichokifanya, na katika zama hizi za sasa, pamejitokeza vitu vipya – vya Kitiba na Uponyaji – vilivyoeneza Balaa, jambo ambalo limepelekea wanachuoni kuliangalia ili wapate hukumu zake za Kisharia kwa namna inayoendana na Maandiko ya Sharia na Misingi yake.

Na miongoni mwa Mambo haya mageni ni “Dawa ya pumu” na ugonjwa wa pumu ni moja ya maradhi yanayotokea katika mfumo wa kupumulia na kupelekea kubana kwa njia ya kupumulia na mwasho wake mkali kutokana na vichochezi maalumu vinavyotutumua njia ya hewa jambo ambalo huongeza ute ute unaolendemka  na ni vigumu kuutoa na kuzuia msukumo wa kawaida wa hewa, na maradhi haya hudhihirika kwa namna ya shinikizo la mara kwa mara ambapo   Pumzi ya mgonjwa hutoka kwa ufinyu sambamba na mruzi unaosikika kisha shinikizo hilo humalizika lenyewe au kwa kutumia dawa.

Na dawa ya pumu ni chombo kinachotumiwa na mgonjwa wa pumu na kina dawa itokayo kwa kupulizwa na upepo ambapo dawa hiyo hutumika kwa dozi aliyoandikiwa mgonjwa ambapo yeye huivuta hewa hiyo mdomoni na huwa inafanya kazi ya kupanua njia ya kupumulia na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Na ina Fatwa yake iliyochaguliwa na jopo la Wanachuoni wa Kisasa ni kwamba Dawa hii ya kupuliza inayotumiwa na mgonjwa wa pumu wakati anapokuwa amefunga Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, inazingatiwa kuwa ni kufungua; na hii inaingia katika ujumla wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku} [AL BAQARAH 187]. [Isiny Al Matwaleb, 415/1]. Yaani ikiwabainishia basi msile na msinywe kitu chochote.

Na yaliyotajwa katika Hadithi Laqitwu Bin Swabrah R.A. kwamba Mtume S.A.W., amesema: Na kuzidisha uvutaji wa maji puani ni sunna isipokuwa kwa yule aliyefunga.[1]

kuzuiwa uzidishaji wa kuyavuta maji kwa aliyefunga ambako kuna ukamilifu wa Sunna ni dalili ya kwamba kuingia maji kooni kunaharibu Saumu ya mtu. [Al Mabswuut 66/3] Na kama sio hivyo, pasingelikuwepo maana yoyote ya kuzuia pamoja na kuwepo amri ya kufanya hivyo kwa asiye kuwa na Saumu, na kwa hivyo kila kinachoingia kooni katika vitu kwa kutaka hivyo kunaharibu Saumu; kwani maana katika yote hayo ni kufika kooni na kutulizana kwake ndani yake pamoja na uwepo wa uwezekano wa kujizuia na hali hiyo kikawaida.

Na kutoka kwa Ibn Abbas R.A., wote wawili, kwamba yeye akasema: “Hakika mambo yalivyo, kinachoharibu Saumu ni kile kinachoingia na sio kinachotoka”[2]

Kama ambavyo maana ya Saumu ni kujizuia, na kujizuia hakupatikani isipokuwa kwa kuzuia kitu chochote chenye umbile kisiingie tumboni, na kama si hivyo basi nguzo ya Saumu itakuwa imekosekana. Na utekelezaji wa ibada bila ya Nguzo zake ni kitu kisichofikirika.

Na kinachotoka kwenye dawa ya pumu ni matone madogo madogo mno yaliyochangsyika na hewa yanayoathiri, na sio kweli kwamba ni hewa tu, na kama hivyo isingelikuwa dawa, kwani hakika mambo yalivyo, hewa tupu anaipumua mgonjwa na asiyekuwa mgonjwa.

Na hiki kinaungwa mkono na kile kilichoandikwa na Waandishi wa Madhehebu Manne yenye wafuasi wengi zaidi, katika hayo ni yale yaliyokuja katika Kitabu cha Badaaiu Swanaaii, miongoni mwa vitabu vya Madhehebu ya Imamu Hanafiy kwa kauli yake: “Na chochote kilichofika tumboni au ubongoni kupitia Matundu mbalimbali ya asili kama vile pua, masikio, na  utupu wa nyuma, kwa kuingiza au kwa sindano au kwa matone masikioni mwake na yakafika sikioni au ubongoni basi Saumu yake itakuwa imeharibika". [Kitabu cha Badaaiu Swanaai' 93/2]

Na Bin Najiim amesema:  “Na maana hasa ya kuacha kula ni kuacha kuingiza kitu tumboni mwa mtu ni muhimu kuliko kuwa kwake kitu hicho kinaliwa au hakiliwi”. [Kitabu cha Al Bahru Ar Ra'eq 279/2]

Na katika Sharehu ya Al Kharshiy Mukhtaswar Khaliili Fii Fiqhi l Maalikiyah: anasema: “Na kusihi kwa Saumu ni kwa kuacha kufikisha Dawa ya majimaji ambayo ni kila kinachopenya kwenye njia ya chini au ya juu au baina ya meno, au kisicho majimaji kama vile dirhamu, kwa kupitia njia ya juu” [Sharhu Al Kharshiy 249/2].

Na katika Matini ya Minhaaj miongoni mwa vitabu vya Madhehebu ya Imamu Shafiy: ni kwamba: "Sharti la Saumu ni kuzuia ufikaji wa kitu chochote ndani ya kile kinachoitwa tumbo" [Kitabu cha: Al Minhaj pamoja Sharu yake Mughniy Al Muhtaaj 155/2].

Anasema Raafiiyu: “Na wanachuoni wamedhibiti kitu kinachoingia na kufuturisha ni kile kinachofika kwa uwazi wake ndani ya tumbo kupitia njia iliyo wazi pamoja na kutaja Saumu" [Kitabu cha: Al Majmuu' 335/6].

Na Bahuutiy mfuasi wa Madhehebu ya Hanbali anasema katika Sharhul Muntahaa: “Au aliingiza kitu tumboni mwake kupitia kila njia inayopitika hadi kufika tumboni mwake kwa hali yoyote ile, kwa maana kwamba:  inavyonzeka na kuwa chakula au hapana, kama vile kijiwe kidogo na kipande cha chuma na risasi na mfano wake, na lau ncha ya kisu kwa kitendo chake au cha mwingine kwa idhini yake basi Saumu yake itakuwa imeharibika. [Kitabu cha: Sharhu Muntaha Al Iradat 481/1].

Na baadhi ya wanachuoni wa kisasa wanaona kwamba mtu aliyefunga anapotumia dawa ya pumu haizingatiwi kuwa inamfuturisha, na wanatoa sababu ya hivyo kwa mambo kadhaa miongoni mwayo ni:

Kwanza: kinachopatikana kutokana na Dawa ya pumu kwa kawaida hakizingatiwi kuwa ni chakula au kinywaji na kwa hivyo hakifunguzi.

Na analizungumziwa jambo hilo kwamba ikiwa huko hakuzingatiwi kuwa ni kula au kunywa kikawaida, basi hakika ya jambo hilo halitoki katika jumla ya vinavyofunguza, na zingatio hapo ni kuingia kwa kitu kooni kwa kutaka; kwa dalili ya Qur'ani na Sunna juu ya kuharamisha kula au kunywa kwa ujumla wake unaokusanya sehemu ya mgogoro.

Na ukweli wa Saumu ni kujizuia, na kujizuia kunapatikana kwa kuzuia kitu chochote kuingia kooni.

Na wanachuoni wameamua kwamba hakuna tofauti baina ya kila kinachojulikana kama ni mila na desturi kama chakula au kinywaji na kile kisichojulikana hivyo. Na Imamu Nawawiy amesimulia katika kitabu cha Al Majmuui, na Ibn Quddaamah katika kitabu cha Al Mughniy kutoka kwa wanachuoni wote na wale walio mashuhuri miongoni mwao katika Watangulizi na Waliokuja baada yao, na hakuna tofauti baina ya Kitu kikavu na kitu chenye majimaji katika mlango huu.

Ya pili: Kuingia Ktiu tumboni kinachotokana na dawa ya pumu sio jambo la kukata shauri kwani kuna uwezekano wa kuingia na kutoingia pia, na asili yake ni kusihi kwa Saumu, na Yakini hii haiondoshwi na Shaka hiyo.

Na kauli hii wanairudi Wanazuoni kwamba imethibiti kwa upande wa kimatibabu kwamba kinachofika tumboni katika dawa kinakaribia kuwa asilimia themanini na kinachobakia kinaelekea kwenye mfumo wa kupumlia, na kwa hivyo kufika kwa dawa tumboni hivi sasa sio jambo linalotiliwa shaka tena, bali ni uhakika, na kinachoondosha  yakini  ni yakini mfano wake.

Tatu: Dawa  ya pumu inaingia kwa njia ya kupumulia na wala sio kwa njia ya kulia chakula au kunywea maji.

Kauli wanazuoni wanairudi kwa kusema kwamba tofauti hii baina ya njia mbili haiathiri chochote; kwani zingatio lililopo ni kufika katika kile kinachoitwa koo bila ya kujali njia ya kuelekea huko.

Nne: kipimo cha dawa ya pumu kinachofika tumboni kwa kulinganisha na kinachobakia baada ya kusukutua na kuvuta maji puani.

Na kipimo hiki ni pamoja na utofautishaji; kwani sehemu inayokusudiwa kwayo kosa juu ya aliye na Saumu hakika mambo yalivyo ni Koo, nalo sio kusudio la kusukutua, bali kinachokusudiwa ni mdomo, kinyume na hali ilivyo katika dawa ya pumu kwani hakika Koo ndilo hasa linalokusudiwa na kulengwa na dawa hiyo.

Na kwa hivyo kupita kwa athari ya kusukutua kooni ni kwa njia ya kimakosa ambayo ni matokeo tu ya uwepo wake; kwani ukamilifu wa kusudio la kitendo ni kwa kukusudia sehemu yake, na katika kosa kuna lengo la kitendo bila ya kukusudia sehemu.

Anasema bin Alhimaamu – akifafanua maana ya kosa - : "Ni mtu kukusudia kitendo kinyume na sehemu ambayo linakusudiwa kosa kutuka". [Kitabu cha At Taqrir Wa Ataheer 204/2]

Na anasema Swadru Shariia: "Ni kufanya kitu bila ya kukikusudia kusudio kamili". [Kitabu cha: At Talweeh Ala At Tawedheeh 389/2].

Na vilevile hakika katika kuchukua tahadhari ya athari ya kusukutua ni aina ya kitu kinachokuwa kigumu pamoja na kuwa kwake kinatakiwa na Sharia katika Usafi (Twahara), na Ugumu unaleta Wepesi. Na Wanachuoni wameshurutisha kutopatikana uvunjaji wa Saumu kwa kutema mate baada ya funda la maji mdomoni; kwa kuchanganyika kwa maji na mate na kwa hivyo hakitoki kwa kutema tu, na wala hakushurutisha kutema kwa nguvu; kwani kinachobaki baada ya kutema ni majimaji tu na unyevu ambavyo huwezi kujilinda  navyo.

 Al Mutawalli kutoka Wafuasi wa Madhehebu ya Shafi amesema:  “Mtu aliyefunga, anaposukutua analazimika kuyatema maji na wala halazimiki kuukausha mdomo wake kwa kitambaa au mfano wake, na hakuna hitilafu yoyote ya Wanachuoni katika jambo hili; kwani katika kufanya hivyo kuna uzito mkubwa, na kwamba hakuna kinacho bakia mdomoni baada ya kusukutua isipokuwa umajimaji usioweza kujitenga na eneo husika; kwani kama ungelikuwa ni wakujitenga basi ungelitoka katika kutema maji ya kusukutulia. [Kitabu cha Al Majmuu' 357/6]

Kipimo cha Dawa ya pumu kwa dawa ya mswaki katika kujuzu kuitumia kwake kwa mtu aliye na Saumu pamoja na kuwepo baadhi ya maada ndani yake ambazo zimeruhusiwa: kwa uchache wake na kwa kuwa kwake sio kinachokusudiwa.

Na hapa panajibiwa kwa jibu lililotolewa na dalili iliyotangulia, vilevile kinachosamehewa ni kile kilichokuwa na ugumu wa kukiondosha, na ama kwa upande wa kile ambacho sisi tunakizungumzia basi kinachokusudiwa ndicho kinachotegemewa.

Imamu An Nawawiy anasema: kama mtu atapiga mswaki kwa mswaki mbichi wenye majimaji na kisha kikatoka kitu katika ubichi huo au kitu katika sehemu ya mswaki na akakimeza basi atakuwa amefungua bila pingamizi, na Faurani pia ameyasema hayo pamoja na wanachuoni wengine wengi. [Kitabu cha Al Majmuu' 343/6]

Sita: Huko hakulingani na kula na kunywa bali kunalingana na kutoa damu kwa ajili ya kuichunguza na sindano hailishi chakula.

Na mwandamamo huu unapingika kwa kuwepo utenganishaji baina ya dawa ya kupuliza ya Pumu na baina ya yale yaliyotajwa; basi hakika dawa ya pumu inatofautiana na utoaji wa damu mwilini kwani ya pumu ni ndani, na hii ni nje, na kufungua kinywa  ni kwa kinachoingia ndani na sio kinachotoka – kama ilivyo kuwa sahihi kutoka kwa Ibnu Abbas Mola awawie Radhi yeye na Mzazi wake – , kwamba Dawa ya pumu ya kupuliza inaingia kooni kupitia njia ya kawaida na utoaji wa damu na ambayo ni Sehemu ya mabaki ya mwili na kwa njia isiyo ya kawaida kuna fanana na kupiga chuku.

Na kuna tofauti kubwa baina ya dawa ya pumu na sindano isiyolishia chakula katika kuwa sindano haifiki tumboni  kupitia Matundu ya kawaida, na katika kukisia ufikaji wa chakula tumboni hakika mambo yalivyo chakula hufika kupitia Mishipa tu na kinachofika huko sio tumboni na wala hakiwi katika hukumu hiyo ya tumboni, na ndipo kilipofananishwa na mfano wa mtu aliyepaka uwanja na akaihisi ladha yake kooni basi hakika haizingatiwi kama inafunguza.

Wanasema Wanachuoni: kilichopo katika koo lake ni athari inayoingia njia ambayo ni mpenyo uliopo mwilini, na kinachofunguza hakika mambo yalivyo ni kile kinachoingia kupitia matundu; kwa makubaliano ya kwamba atakayeoga katika maji na akaipata baridi ya maji hayo tumboni mwake basi huyo hajaharibu Saumu yake. [Kitabu cha Radu Al Muhtaar 395,396/2]

Baada ya hayo, iwapo itaamuliwa ya kwamba dawa ya pumu ni katika vitu vinavyoharibu Saumu, basi hakika mtumiaji wake hawezi kuepuka kuwa kwake mgonjwa mweye ugonjwa wa muda mfupi au mgonjwa wa ugonjwa wa kudumu. Na ikiwa mjonwa atakuwa na sifa ya awali ambayo ni ugonjwa wa muda mfupi ambao unatazamiwa kupona, basi analazimika kulipa pale anaweza kufunga Saumu. Na hayo kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na mwenye kuwa mgonjwa ausafarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine}. [AL BAQARAH 185]

Na kwa upande wa mgonjwa asiyetarajiwa kupona kwa sababu ya ugonjwa wake kuwa sugu basi atafungua na atakula chakula na hadaiwi Saumu; Kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Walahakuweka juu yenu mambo mazito katika Dini} [Al Haj 78] analazimika kutoa fidia kila siku kwa kulisha maskini mmoja kwa kiasi cha pishi moja ya chakula kilichozoeleka. Na pishi moja ni sawa na gramu 510, na inajuzu kutoa hata fedha zenye thamani ya hiyo pishi moja ya chakula kwa masikini kwa mujibu wa Fatwa yao.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

Imeandikwa na Ahmad Mamduoh.

 

[1] - [Imesimuliwa na Abu Dawud 142, na At Tirmiziy 788, na wengineo, na At Tirmiziy akasema ni hadithi nzuri na sahihi].

[2] - Al Bokhariy katika mlango wa "Al hujamah wa Al Qai' kwa Mwenye Saumu" na Ibn Ani Shaibah akaitaja katika Musnad yake, 467/2, na Al Bahaiqiy katika sunan zake, 116/1,  kutoka kwa Ibn Abbas ikisimamishwa, na An Nawawiy akisahahisha katika kitabu cha Al Majmuu' 340/6

Share this:

Related Fatwas