Hukumu ya Kutumia Sindano Wakati wa...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Kutumia Sindano Wakati wa Saumu

Question

Hukumu ya Kutumia Sindano Wakati wa Saumu

Answer

Saumu ni ibada tukufu zaidi kuliko ibada zote, ambazo Mwenyezi Mungu Mtukufu alizifaradhishia Umma. Basi Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Enyi mlio amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyoandikiwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kuchamngu}. [AL BAQARAH 183] Na Mtume Mkarimu S.A.W. aliizingatia ni moja miongoni mwa nguzo za Uislamu ambazo umejengewa, kama alivyosimuliza Ibn Omar R.A wote wawili akasema: Mtume S.A.W. Amesema: "Uislamu ulijengwa juu ya nguzo tano; Shahada kwamba hakuna Mola yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Mohammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kusimamisha Swala, Kutoa Zaka, kuhiji, kufunga Mwezi wa Ramadhani"[1]

Wanachuoni wamezungumza pale walipozishughulikia hukumu za Saumu na vitenguzi vyake na wakakubaliana baadhi na wakatofautiana na baadhi ya vingine, na katika walitofautiana ni hukumu ya kutumia sindano wakati wa Saumu.

Na neno la kufungwa sindano linamaanisha kuingiza kimiminika mwilini kwa njia ya tundu la haja kubwa kwa kuingiza sindano.

Sindano ya kupitishwa kwa njia ya haja kubwa ni chombo cha kimatibabu ambacho kwacho kupitishwa vimiminika katika uti wa mgongo na utumbo mkubwa kwa njia ya tundu la haja kubwa na hutumika kwa malengo maalumu ya kimatibabu kama vile kutibu ugonjwa wa choo kigumu kama sehemu ya tiba mbadala, au kwa njia ya misuli, ambayo watu sasa wanaiita sindano.

Unapozungumzia sindano katika vitabu vya Fiqhi unakusudia kile kifaa chenye ncha ambacho huingizwa kwa njia ya haja kubwa na wala sio sindano inayotumika kufikisha dawa au chakula kupitia mishipa ya damu au kwa njia ya misuli ya mwili, (Mikononi au matakoni) na ambayo watu hivi sasa kwa pamoja wamezoea kuiita sindano.

Tofauti kati ya mishipa ya damu, mikubwa na midogo

Mishipa mikubwa ya damu ni mirija ya damu inayosafirisha damu yenye oksijeni chache na kuifikisha katika moyo, na mishipa midogo ni ile inayoihamisha damu yenye oksijeni kutoka moyoni na kuipeleka katika Sehemu mbalimbali za mwili.

Na katika yaliyofuata tunaweza kueleza maelezo ya suala hilo katika milango miwili:

Wa Kwanza: Kutumia sindano katika mshipi wa msuli kwa lengo la kutiba au chakula.

Wa Pili: kutumia sindano katika njia ya haja kubwa, kwa malengo ya kutiba au mengineyo.

Mlango wa Kwanza

Kutumia Sindano Katika Mshipi au Misuli

Tunachokitegemea kwa ajili ya Fatwa ni kwamba matumizi ya sindano wakati wa Saumu kwa njia ya mshipa wa damu ndani ya ngozi au chini yake sio lazima kuharibu Saumu, na inalingana katika hali hiyo na pale sindano hiyo inapotumika kwa ajili ya kuingiza chakula au dawa mwilini. Na hivi ndivyo walivyofutu wanachuoni wengi, kama vile, Mhakiki mkubwa Mwanachuoni Mbobezi, Sheikh Muhammad Bakhiit Mutwii-ii, na Shekh Abdulmajeed Seleem, na Shekh Hasan Ma'muon, rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ziwe juu yao wote wawili.

Na hili inamaanisha kwamba Makubaliano yamepatikana kwamba mtu atakayezamia majini na akaihisi baridi ya maji hayo ndani ya mwili wake, hakika mambo yalivyo hali hiyo haimfunguzi; ni kana kwamba kinachozingatiwa katika kupatikana ufunguzi ni kufika kwa kitu ndani ya mwili kupitia matundu yaliyozoeleka, ama kwa kile kinachoingia mwilini kupitia vimelea vya mwili hakika sheria haikizingatii na wala haikihesabii kuwa ni katika vifunguzi.

Na sindano iliyotajwa katika maana hiyo hiyo; hakika kinachofikishwa ndani ya mwili hakifiki isipokuwa kupitia njia iliyo wazi mwilini kwa kuingiza sindano katika njia hiyo. Na hiyo imefanikiwa na sura ya mwenye kuzamia majini.

Na katika maana hii pia kuna tamko la wanachuo ni kwamba mtu yeyote atakayepaka wanja au tone la dawa machoni mwake kisha akahisi ladha yake kooni basi ladha hiyo haitamfunguza.

Na katika yafuatayo baadhi ya matini za mafakihi ambayo yanathibitisha hayo:

Imamu Ibn Abdiin alisema katika kitabu cha: [Hashiyat Ibn Abdiin] kwenye tamko la mwenye kitabu cha: [Ad Duru Al Mukhtaar]: "(Na ikiwa atahisi ladha yake kooni): Kwa maana ya ladha ya wanja, au mafuta kama ilivyo katika Kitabu cha: [Siraaj], na pia kama atatema mate na  kwa usahihi akaipata rangi ya bahari. Na amesema katika Kitabu cha: [Nahr]: kwamba  kilichopo katika koo lake ni athari ndani ya matundu madogo madogo ambayo ni mianya ya mwili, na kinachofunguza hakika mambo yalivyo, ni kile kilichoingia kupitia matundu au njia, kwa makubaliano ya kwamba mtu yeyote atakayeyaoga maji na akaihisi baridi yake ndani ya mwili wake, basi hiyo haitaharibu Saumu yake, isipokuwa Imamu ameona kuchukiza kuingia kwenye maji au kujigubika shuka iliyolowanishwa maji kutokana na kudhihirisha kwake kemeo la kutofanya hivyo wakati wa kutekeleza ibada, sio kwa sababu ya kufunguza". [Hashiyat Ibn Abdiin juu ya  Ad Duru Al Mukhtaar, 395-396/2 ]

Na imetajwa katika kitabu cha: [Al Minhaaj na Sharhu yakep kitabu cha: Nihayatu Al Muhtaaj kwa Mbobezi Ar Ramliy, miongoni mwa vitabu vya wanavyuoni wa Kishafi: "(Na sharti la kufika ni kuwa kwake katika njia) kwa maana ya Sehemu ya kuingilia au kutokea (iliyowazi basi haidhuru kwa kuingia mafuta) na kufikia tumboni (yananywea kwenye vitundu vidogo vidogo vya mwili), na wala haidhuru kujipaka wanja hata kama mtu ataihisi ladha yake) kwa maana ya ladha ya wanja (kooni mwake) kama ambavyo haidhuru kuzamia majini hata kama atapata athari za maji katika tumbo lake; kwani Mtume S.A.W, alikuwa anapaka wanja hali ya kuwa ana Saumu, basi haina karaha kwa kupaka wanja na matundu madogo madogo ambayo ni mianya ya mwili". [Kitabu cha Nihayatu Al Muhtaaj 168/3]

Na kuhusu yaliyosemwa: kwamba kutumia sindano ya chakula kunaharibu Saumu; ni kwa kuwa sindano hukifikisha chakula katika viwango vyake vya juu kwa namna ambayo hufika moja kwa moja kwenye damu, na aliyefunga wakati huo huhisi kuchangamka, na jambo hili linakinzana na lengo la Saumu.

Basi jibu lake ni: Hakika kwamba Uhalisia wa Saumu ni kujizuia na kufika kitu chochote kisichokuwa cha mwili yaani kutoka nje ya mwili wa mtu, hadi kufika ndani ya tumbo la aliyefunga, na hili ndilo ambalo sharia imeliona kuwa linasababisha kupatikana kwa ufunguzi wa Saumu kwalo na ikaweka katika mazingatio, na Sharia haijamshurutisha mfungaji kwamba lazima awe amekula.

Na hali ya kuwa Mfungaji ana njaa au ana kiu, hakika mambo yalivyo, hiyo ni katika Hekima za  kufunga; ili amhisi wengine wenye shida na wenye kuhitaji msaada, na wala sio sababu ya kufunga kiasi kwamba vinapokosekana basi na Saumu inaharibika au haipatikani, bali mtu anaweza kufunga Saumu na akawa hajaathiriwa na njaa au kiu na Saumu yake ikawa sahihi kabisa pamoja na hayo yote.

Kama inavyokuwa Sindano hii haiwezi kusababisha upatikanaji wa kile kinachopatikana kwa kula na kunywa kama vile ladha na matamanio na kula kikamilifu na kujaza tumbo, na ndio maana utakuta mtu anayelishwa kwa mirija anakuwa na hamu kubwa ya kutaka kula na kunywa, na anahisi kwamba mirija hiyo au sindano haikumfanya aache kula na kunywa.

Mlango wa Pili

   Sindano ya Kuingiza Dawa Kupitia Tundu la Haja Kubwa

Tumesema hapo kabla ya kwamba matumizi ya vitabu vya zamani vya Fiqhi vinavyozungumzia sindano kinachokusudiwa kwa maana hiyo hivi sasa ni kuingiziwa mirija; kwani kisichokuwa hicho hakikuwa kikijulikana katika zama hizo, na wala sindano hazikutumika enzi hizo, na hivi sasa kinachoitwa sindano wakati huo kilikuwa na maana ya kuingiza dawa kupitia tundu la haja kubwa   .

Na miongoni mwa matini za kifiqhi zinazothibisha hayo:

Tamko la Al Hadadiy katika kitabu cha: [Aj Jawharah An Nairah] kutoka vitabu vya wanazuoni wa kihanafi, (kujidunga) maana yake ni kumiminika dawa katika tundu la haja kubwa. [Kitabu cha Aj Jawhara An Nairah 141/1]

Na Al Kharashiy Al Malikiy alisema: " Na sindano hii hutumika kutibu mshipa wa upepo au ugonjwa wowote ulio katika utumbo ambapo dawa humiminwa humo kupitia tundu la haja kubwa kwa chombo maalumu, na hapo ndipo dawa inapofika utumboni, na chakula kinachofika kwenye utumbo huleta faida ya chakula; kwani ini hujivuta kutokana na mfuko wa chakula na  matumbo yote kwa mujibu wa Madaktari, na kwa hiyo ndio maana ya kula chakula, naye Sand amesema hivyo na ametumia kizuizi kujikinga na kitu Kigumu , basi hapo hakuna kulipa Saumu". [Kitabu cha: Sharhu Al Kharashiy juu ya Mukhtaswer Khalil, 249/2

Na Mbobezi Al Khatweeb As Sherbiny alisema: "Sindano (kudunga) ni kuingizia dawa  au  shabaha yake kupitia tundu la haja kubwa". [Kitabu cha Al Iqnaa 380/2, pamoja na Hashiyat Al Bigermiy]

Na hicho kinachoitwa Sindano ya Utupuni, mrija au bomba la kuingizia dawa kupitia tundu la haja kubwa, na ni katika vinavyomfunguza aliyefunga ambapo atalazimika kulipa siku alizokula, awe mtu huyo alitumia njia hiyo kwa ajili ya matibabu au kwa ajili ya kitu chochote kingine, kwa sababu hiyo sindano hufikisha mmiminiko hadi tumboni kupitia njia ya tupu la haja kubwa iliyowazi, na kinachofika tumboni kupitia njia iliyowazi husababisha kufunguza.

Kutokana na Hadithi ya Laqiiytw Bin Swabrah ambaye alisema: Mtume S.A.W. amesema: "Chukua udhu wako vizuri (yaani kila kiungo ukioshe vyema), na uvichambue vidole vyako vizuri na uzidishe katika kuvuta maji puani, isipokuwa unapokuwa kwenye Saumu”.[2] Na akamuepusha mfungaji katika kuzidisha uvutaji wa maji puani ingawa hiyo ni sababu za kuikamilisha Sunna yake vyema; kwa kuchelea maji yasije yakafika kooni au tumboni mwake kwa kuzidisha huko katika kuyavuta puani na ikapelekea kuharibu Saumu yake na hiyo ikawa inamaanisha kwamba kila kilichofika tumboni kwa hiari yake mtu kinamfunguza Mfungaji. Na kutoka kwa Ibnu Abbas R.A, wote wawili amesema: “Hakika kinachofunguza ni kile kilichoingia sio kilichotoka.” [3]

Na wanazuoni wa madhehebu nne waliafikiana kwamba sindano ya kupitia katika tundu ya haja kubwa ni miongoni mwa vitu vinavyofunguza, na mtu anayechukua analazimishwa kulipa Swaumu yake.

Al Kassaniy akisema katika kitabu cha: Badaai' As Swanae' kutoka vitabu vya Wanazuoni wa Kihanafi: Na kinachofika tumboni au ubongoni kupitia matundu ya asili kama vile pua, sikio, na tupu ya nyuma ni kwamba mtu alijimezea au alijidunga au alijidondoshea matone matone sikiona mwake na vikafika hadi tumboni mwake au ubongoni mwake basi Saumu yake itakuwa imeharibika. [Badae' As Swanae' 93/2]

Na Mbobezi Al Kharashiy wa kimaliki alisema katika sharhu yake kwa kitabu cha: [Mukhtaswar Khalil], Na kuifikisha dawa au kitu chochote kingine tumboni kama ilivyochaguliwa, kwa kutumia mrija kwa kimiminika au kooni) na kusihi kwake- kwa maana ya Swaumu: kuacha kufikisha Kimiminika nacho ni kila kinachoweza kuingia kupitia tundu la juu au la chini la mdomoni isipokuwa kinyume na kati ya meno ya juu na ya chini au kisichokuwa kimiminika kama vile Dirham kupitia njia au tundu la juu kama inavyokuja kuelezwa kama alivyochagua Lakhamiy maana ya kutoka, na maana yake hasa ni: kufikisha kimiminika tumboni mwake nacho ni kile kilichopenya kutoka kifuani hadi kitovuni kwa sababu ya kudungwa sindano au kutowa mirija au bomba kupitia njia ya haja kubwa au utupu wa mbele wa mwanamke na wala sio kwa njia ya haja ndogo kutokana na kizuizi na ikiwa atafanya kitu kama hicho, basi kauli iliyo mashuhuri ni kulipa Saumu yake” [Sharhu Mukhtswar Khlil kwa Al Kharashiy 249/2]

Naye Sheikh wa Uislamu, Sheikh Zakaria Answaari amesema: Na sindano inayofunguza ni sindano za dawa maalumu zinazojulikana kwa maana ya kufika kwake tumboni" [Kitabu cha Isniy Al Matwaleb 416/1]

Na Al Bahutiy akasema katika kitabu cha: [Sharhu Al Muntaha]: "Mwenye Saumu anapokula au kunywa au akapaka mafuta katika pua yake au kitu kingine chochote, na kikafika katika koo lake au ubongo wake  - na katika Kitabu cha Alkaafiy: hadi katika matundu yake ya ndani ya pua – basi Saumu yake itakuwa imeharibika (au alichoma sindano au alitibu kidonda kilichochimbika na dawa ikaingia ndani ya tumbo lake, basi kwa kauli ya wanachuoni, Saumu yake itakuwa imeharibika”  [Kitabu cha Sharhu Muntaha Al Iradat 481/1]

Na kundi la Wanachuoni wameona kwamba kudunga sindano kupitia tundu la haja kubwa haisababishi kufunguza Saumu, miongoni mwao Al Hassan Bin Swaleh na Dawud Adh Dhaheriy, [Kitabu cha Al Majmou' 346/6] na Al Qadhi Husain kutoka wakishafiy [Kitabu cha Al Majmou' 335/6]  na Sheikh Taqiy Ed Deen Bin Taimiyah.

 Na Ibnu Taimiyah ameeleza sababu mbalimbali za jambo hili kwa kusema: “ Hakika Saumu ni katika Dini ya Waislamu ambayo lazima ieleweke vyema na kwa watu maalumu na kwa watu wote , na kama mambo haya yangelikuwa miongoni mwa yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika Saumu na yanafunguza Saumu kwayo basi hilo lingekuwa ni katika mambo ya lazima kwa Mtume S.A.W, kuyabainisha, na kama Mtume S.A.W. angelizungumzia jambo hili, basi Maswahaba wake wangekuwa wanalijua vizuri na wangelifikisha kwa Umma kama walivyoifikisha Sharia yake yote.

Na kwa kuwa hakuna yeyote miongoni mwa wanachuoni aliyenukulu kutoka kwa Mtume S.A.W, sio Hadithi Sahihi, au Hadithi Dhaifu, au Hadithi iliyo Musnad au Hadithi iliyo Mursal – inajulikana ya kwamba hakuna chochote  kilichosemwa kuhusu jambo hilo mpaka aliposema: "Hakika vitu hivyo vinafunguza kama vile kudunga sindano au kuingiza bomba au mrija na kutibu kidonda kilichochimbika hadi ubongoni na jeraha lililofika tumboni, hawakuwa na hoja yoyote kutoka kwa Mtume S.A.W, bali hakika wao wamesema hivyo kulingana na Kipimo walichokiona wao, na Kauli yenye nguvu zaidi ambayo waliitumia kama hoja ni ile aliyosema Mtume S.A.W, na uzidishe katika kuvuta maji puani isipokuwa unapokuwa kwenye Saumu".

Wakasema: hayo yanamaanisha kwamba kinachofika ubongoni kinamfunguza Mfungaji ikiwa kinatokana na kitendo chake yeye mwenyewe kama vile kuchomwa sindano na vinginevyo. Iwe ni katika sehemu ya kuingizia chakula au kwa njia nyingine yoyote ile ya kujaza chakula tumboni mwake. [Kitabu cha: Majmou' Al Fatawa 234/25]

Matamko hayo yanajadiliwa katika yafuatayo:

Kauli yake: Saumu ni katika Dini ya Waislamu ambayo inahitaji kuelewekwa na watu maalumu na watu wote. Na kisichokuwa na mjadala ni kwamba Saumu inahitajika kueleweka kwa watu wote kwa kuwa kwake ni Faradhi, ama kuhusu masuala mbalimbali na hukumu zake haishurutishwi kwa watu wote kuyajua. Na haifichiki kwa mtu kama Ibnu Taiminyah kwamba hukumu nyingi za matawi zinazofungamana na Saumu na mambo mengine zinaweza kuwa zimefichikana kwa Waislamu walio wengi. Na iliwahi kutokea hitilafu baina ya Maswahaba na waliokuja baada yao miongoni mwa Wanazuoni na Wenye kujitahidi katika masuala mbalimbali ya Saumu kwa kufuata hitilafu za wenzao.

Kauli yake: Kama mambo haya yangelikuwa miongoni mwa yale aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake katika Saumu na yanafunguza Saumu kwayo basi hilo lingekuwa katika yale mambo ambayo Mtume S.A.W, analazimika kuyabainisha kwa Umma. Kuyarudi maneno ya kwamba sisi tunazuia kuwa Mtume S.A.W, hajawahi kuyafafanua hayo, na imetangulia katika kutaja maana zinazomaanisha wito wetu na ambazo Wanachuoni wengi wamezitegemea katika yaliyotangulia, na miongoni mwayo ni yale yaliyotajwa na Sheikh Ibnu Taiminyah yeye mwenyewe kutokana na uwazi wa Kipimo ndani yake.

Katika Kauli yake S.A.W: “Na uzidishe katika kuvuta maji puani isipokuwa kama utakuwa na Saumu “. Na si sharti kwamba kuelezwa Hukumu kwa kila mtu miongoni mwa watu wa matukio katika Matini za Kisharia bali kuna uwezekano wa kunufaika na Hukumu zake na pakagundulika mambo ya jumla au kwa aina za sababu zilizojificha kama vile maana ya ishara na mfano wake.

 Kauli yake "kama aliyasema hayo basi Maswahaba wangeyajua na wangeyafikisha kwa Umma kama walivyoifikisha Sharia yake yote, na kwa kuwa hakuna yoyote miongoni mwa wanachuoni aliyenakili kutoka kwa Mtume S.A.W, katika hayo, hakuna Hadithi yoyote Sahihi au Dhaifu au Musnad au Mursal – inakuwa imejulikana kwamba hakuna kitu chochote kilichotajwa katika hayo"

 Tunasema: Ama kilicho Sahihi ni kuwa hawakuijua na hawakuielezea kwa hiyo hiyo ni Hadithi inayokataliwa, na sisi tunategemea ujumla wa kauli ya Ibnu Abas Katika Hadidhi ambayo ni Sahihi kutoka kwake: “Kinachofuturisha ni kile kilichoingia tumboni “ na imenukuliwa kutoka kwa wengine miongoni mwa wema waliotangulia na Taabiina kwamba sindano inaruhusiwa , kwani Atwaau aliulizwa: Je mtu anaweza kuingiza kitu? Akasema: hapana. Na Shaabiyu aliulizwa: kuhusu kudungwa sindano kwa mtu aliyefunga: akasema: “Mimi ninachukia hicho kitu kufanyiwa mtu asiyefunga, sembuse kwa yule aliyefunga”, [Ibn Abi Shaibah alizisimulia 464-365/2, katika malango wa Kudunga sindano kwa mfungaji] nacho ndicho alichokinukulu Imamu Abu Said Mutawalli kutoka kwa Wanachuoni wa Madhehebu ya Shafi ukiachilia mbali Wanachuoni walio wengi. [Kitabu cha: Al Majmou' 346/6]

Ama tamko lake: "Na wale waliosema kwamba vitu hivi vinaharibu Saumu kama vile kudunga sindano na kutibu Jeraha la Kichwani (linalofika kwenye ngozi nyepesi ya ubongo) na Jeraha la tumboni (linalopenya hadi ndani), hawakuwa na hoja yoyote kutoka kwa Mtume S.A.W,." Na hakika imebainika ubatili wa kauli hii kama ilivyokwisha tajwa hapo kabla.

Kauli yake: "Hakika mambo yalivyo, wao wamesema hivyo kwa kuzingatia Kipimo" Hakika hii ni katika kauli zake za kushangaza mno;  Hakika Kipimo ni katika jumla ya Dalili mbalimbali zitumikazo katika kutafuta Hoja mbalimbali, na hakwenda kinyume katika utoaji wake wa hoja isipokuwa wachache katika wafuasi wa Madhehebu ya Dhwaahiriyah na walioelekea mwelekeo wao, na hukumu nyingi hazina dalili zozote isipokuwa Kipimo.

Na Sheikh Ibnu Taiminyah ni katika wanaosema hivyo, na akawa anamsifu pale anapotaka kuthibitisha madai yake kwa kutengua Dalili inayoenda kinyume naye, ili atengue Kipimo chake kwa moja ya hoja tenguzi zinazojulikana katika Elimu ya Kujadiliana na Elimu ya Usuul,  na sio yeye kuleta maelezo ambayo uwazi wake unafikirisha kutozingatia Kipimo jambo ambalo linakinzana hata na Akida yake mwenyewe.

Kauli yake: "Na hoja kubwa waliyoitumia ni kwamba Kauli yake: uzidishe katika kuvuta maji puani isipokuwa unapokuwa na Saumu", na hii ni katika kauli wanazozirudi wanachuoni kwa maneno yake yaliyotangulia kwamba hakuna yoyote miongoni mwa wanachuoni aliyenakili kutoka kwa Mtume. S.A.W., katika jambo hilo, hakuna Hadithi Sahihi, au Dhaifu au Musnad au Mursal.

Isipokuwa iwe aliitaka Hadithi inayomaanisha kinachotakiwa kwa umaalumu wake, na kushuritisha jambo hili ni kutokana na ulazima wa Sehemu; kwani Hadithi zina mzingiro maalumu na matukio hayana mwisho, kama tusingelitumia Kipimo na Kuangalia hatuwezi kuuweka mlango wa Kuzijua Hukumu za Majaribu na Matukio Mapya, jambo ambalo linamaanisha upungufu wa Sharia  - na hili liko mbali.

Na Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi Zaidi

[1]- Wanaafikiana juu yake, imetolewa na Al Bukhariy, katika kitabu cha: Al Imaan, mlango wa: Uislamu Umejengwa nguzo tano, hadithi Na. 8. Na Muslim katika kitabu cha Al Imaan, malngo wa "Kubainisha nguzo za Uislamu, hadithi Na. 18

[2] - Ilitolewa na Abu Dawud katika kitabu cha: [At Twharah] mlango wa (Al Istinthaar) kutoa maji puani, Hadithi Na. 142. Na At Tirmiziy katika kitabu cha: [Swaumu] mlango wa yalitajwa katika ukaraha ya uzidishi katika kuvuta maji puani kwa mtu mwenye Swaumu, hadithi Na. 788, na akasema: hiyo ni hadithi sahihi, na wanazuoni wamekarahia uzidishi kuvuta maji puani kwa mwenye Swaumu. Na waliona kwamba hayo yanamfunguzia. Na katika mlango dalili za kuimarisha tamko lao. Na Imamu An Nawawiy aliisahihishia katika kitabu cha [Al Majmou'.

[3] - Al Bokhariy aliielezea katika malngo wa Hujamah na kutapika kwa mwenye Swaumu, Na Ibn Abi Shaiba aliitajia katika kitabu cha Al Muswanaf467/2, Na Al Baihaqiy katika Sunan zake 166/1 kutoka kwa Ibn Abbas imewakifiwa, Na An Nawawiy aliisahihishia katika kitabu cha Al Mjmuo' 340/6, Na Abu Ya'ely aliisimulia katika Musnad yake 211/10. Imeinua kutoka kwa Aisha R.A. kwamba alisema: Mtume S.A.W. aliingia kisha akasema: Ewe Aisha, je kuna kipande cha mkate? Nikamletea kipande kidogo sana cha mkate na akakiweka mdomoni mwake na akasema: Ewe Aisha, je kipande hicho kimeingia chochote katika hicho tumboni mwangu? Vivyo hivyo busu la mtu aliye na Swaumu, hakika mambo yalivyo, ni kwamba kinachofunguza ni kile kinachoingia na wala sio kinachotoka, na amesema Baihaqiy kuhusu Hadithi yenye Hukumu ya Marfuu: kwamba haithibiti 

Share this:

Related Fatwas