Hukumu ya kufuatilia na kupeleleza ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kufuatilia na kupeleleza aibu za watu

Question

Ni ipi hukumu ya kufuatilia na kupeleleza aibu za watu na kutafuta dosari zao?

Answer

Mtume (S.A.W.) alitahadharisha waislamu vikali kutokana na hatari na uovu wa kuzungumzia aibu za watu na kuvunja heshima zao na kupeleleza pungufu zao, akimwonya anayefanya hivyo kuwa kwa kitendo hiki huwa anakaribia kufichua aibu zake mwenyewe akiendelea kuwa na tabia hiyo, na kwamba anayevunja heshima za watu atapatwa na adhabu ya aina hiyo hiyo kwa kuvunjiwa heshima na kutiwa aibu na Mwenyezi Mungu hata akijificha humo nyumbani mwake, imesimuliwa na Thawban (R.A.) kwamba Mtume (S.A.W.) alisema: “Msiwaudhi waja wa Mwenyezi Mungu, wala msiwatie aibu, wala msifuatilie aibu zao, kwani anayefuatilia aibu za nduguye Muislamu, basi Mwenyezi Mungu Atafichua aibu zake hata akijificha nyumbani mwake” (imesimuliwa na Ahmed)

Na tabia hii ni aina ya upelelezi unaokataliwa, ambapo Mtume (S.A.W.) alitahadharisha vikali kutoka tabia hii na kutokana na tabia yoyote inayoharibu husiano zilizopo kati ya watu na kusababisha kuenea kwa chuki na bughudha, kwa mujibu wa Hadithi nyingi ikiwemo Hadithi ya Abu Hurairah (R.A.) kutoka kwa Mtume (S.A.W.) alisema: “Epukeni na kuwatuhumu watu, kwani tuhuma ni maongezi yaliyo mabaya zaidi, wala msitafute habari za watu, wala msipeleleza, wala msihusudiana, wala msigombana, wala msichukiane, bali muwe waja wa Mwenyezi Mungu wakiwa ndugu” (Imekubalika na wote)

Share this:

Related Fatwas