Hukumu ya kufurahia kifo cha mtu

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kufurahia kifo cha mtu

Question

Ni nini hukumu ya kufurahi kwa kifo cha mtu mwingine

Answer

Kufurahi kwa msiba wa mwingine ikiwa kifo au shida yoyote nyingine ni mbaya na sifa inayochukiwa kwa hiyo haikubaliki kisheria, hivyo tabia hii inakataliwa katika Sharia ya Kiislamu, kwani ni tabia mbaya inayochukiza kwa nafsi iliyo na mwenendo mzuri, na wenye huruma na utu huikataa, imepokelewa na Wathila bin Al-Asqa'a (R.A.) kuwa Mtume (S.A.W.) amesema: "Usioneshe furaha yako kwa msiba wa ndugu yako akaponywa ukapatwa na balaa yake wewe" imesimuliwa na Al-Termidhiy.

Kwa kweli, maumbile ya maisha ni kwamba mwanadamu hawi na hali hiyo hiyo milele, bali hali yake hubadilika badilika wala haidumu kwa hali hiyo hiyo, bali huishi katika hali tofauti tofauti kati ya huzuni na furaha, pia, mauti ni miongoni mwa majaliwa ya Mwenyezi Mungu juu ya viumbe wake wote, ambapo wanadamu wote watakufa, kwa hiyo haijuzu kwa mmoja afurahie kifo cha mwenzake kwani bila shaka wote watakufa wala hakuna pa kukimbilia kutokana na kifo japokuwa ataishi kwa muda mrefu, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Kila nafsi itaonja mauti} [Al-Imran: 185]

Share this:

Related Fatwas