Hukumu ya kukufurisha ni ya mahakamani
Question
Kwa nini hukumu ya kukufurisha ni hukumu ya mahakamani?
Answer
Kuhukumu ukafiri ni hukumu ya mahakamni; kwa kuwa hukumu hiyo hufuatana na mambo na mabadiliko mengine kuhusiana na mali, kinga ya damu, kulinda haki na kinga ya Uislamu, kwa hiyo jambo hilo si jambo rahisi, bali ni jambo nyeti na fitina kubwa inayotishia usalama wa watu na jamii nzima, na kwa kuwa asasi zilizo mbali na mahakama hazina uwezo wala ujuzi wa kutekeleza taratibu za kuhakikisha upatikanaji wa masharti ya kutoa hukumu ya kukufurisha au kuvunjika kwake na kutofaa kwake, kwani asasi hizo hazihusiki kwa upelelezi wala haizina mamlaka ya kuingilia jambo hilo lililo hatari, kwa hivyo mahakama ndiyo asasi inayohusika kuamua hatima ya anayehukumiwa ukafiri kwa niaba ya mtawala, ambapo kadhi / hakimu ndiye anayewakilisha umma katika hukumu, hivyo inampasa kutekeleza kazi yake kwa lengo la kuzuia umwagaji damu na kulinda haki na jamii kutokana na fitina na ufisadi, pia majukumu ya hakimu hujumuisha kulinda jamii kutokana na upotofu, fujo na migawanyo.