Mashirikiano ya wakufurishaji na mw...

Egypt's Dar Al-Ifta

Mashirikiano ya wakufurishaji na mwanamke.

Question

Ipi nafasi ya mwanamke kwenye makundi ya kigaidi?

Answer

Makundi ya kigaidi yanamtumia mwanamke matumizi mabaya ili kufikia masilahi ya kidunia na malengo mangine, ambapo wadanganywa wanawake na wasichana Waislamu – kama vile wanaume na wavulana – kujiunga na makundi hayo ya fikra potofu na ukiukaji wa kiimani kibinadamu kwa ajili ya kueneza nguvu maeneo ya dunia na kudai kusimamisha dola ya Kiislamu na kujipa nafasi wao wenyewe kuwa ndio walinzi wa Waislamu duniani, wao wakiwa kinyume na Uislamu dini ya amani usamehevu na upole, na wanamzingatia mwanamke ni kuvunjiwa zaidi haki za kibinadamu kwa upande wa makundi ya kigaidi hasa kundi la “isis” la kigaidi ambapo wanawake kwao wanafikwa na mwisho wa kutekwa kuuwawa kuchapwa viboko na kupigwa mawe, mtandao wa “isis” wameongeza ubaya wao kwa kurudisha vitendo viobu kwa wanawake.

Mwanamke katika maeneo yanayoshikiliwa na mtandao unaotokana na Al-Qaida au mtandamo wa isis ana matatizo zaidi, kwani ni mwenye kulazimishwa kutotoka kwenye nyumba yake isipokuwa kwa kuwepo mtu wake wa karibu, vile vile wanawake wanafikwa na uwepo wa polisi wa wanawake wakiwa wanajifanya ni katika kundi la wanawake ambalo linafuatilia wanawake katika maeneo ambayo yanashikiliwa na makundi hayo, na kundi hilo linafanya kazi ya kusimamia mwenye kwenda kinyume na sheria ambazo zimewekwa na vikundi hivyo.

Share this:

Related Fatwas